Hali ya maambukizi
ya ugonjwa wa malaria nchini imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2007
hadi mwaka 2008 mpaka kufikia asilimia 10 kwa mwaka 2012 na 2013.
Takwimu hizo
zimetolewa hii leo Jijini Dare es salaam wakati wa makabidhiano ya dawa za
malaria zenye thamani ya shilingi Bilion 2 kutoka China,
Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dr Hussein Mwinyi amewataka wazazi
kuhakikisha familia nzima inatumia vyandarua vilivyowekwa dawa ili
kupambana na ugonjwa huo, hayo ameyasema wakati akipokea msaada huo
Pia amewataka
watanzania kufuata maelekezo wanayopewa na wataalam wa afya na
kuongeza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa za Malaria nchini ni nzuri
lakini changamoto ipo katika suala la usambazaji kwenye zahanati
zilizo katika maeneo yasiyofikika hasa vijijini
Hatahivyo serikali
ya china imeendelea kuisaidia tanzania kwa dawa za maleria tangu
mwaka 1968 ikiwa ni miaka 45 sasa, pia Waziri ameishukuru serikali ya
china kwa ushirikiano wao ambao unachangia kwa kiasi kikubwa katika
kutokomeza ugonjwa huo
EmoticonEmoticon