NSSF YALIA NA UNIVERSAL PENSION, WAWATAKA WADAU KUJIRIDHISHA KABLA YA KUIPITISHA, SASA KUJITOSA KUKOMESHA MALERIA

Shirika la taifa la hifadhi ya jamii NSSF imewatahadharisha waajiri wasiowasilisha michango ya kila mwezi ya wafanyakazi ambao wamejiunga katika mfuko huo, na kuahidi kuwachukuliw hatua za kisheria pamoja na kulipa faini ya kipindi chote ambacho hawakuwasilisha fedha hizo.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam Meneja kiongozi wa uhusiano na huduma kwa wateja Bi Eunice Chiume amesema waajiri wanatakiwa kuwasilisha michango ya wanachama wao kwa wakati na kuongeza kuwa asiye fanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria

Aidha, NSSF imedhamiria kuwawezesha wanachama wake kwa mikopo kupitia SACCOS ambapo Bi. Eunice Chiume amesema kisheria NSSF haitakiwi kukopesha wanachama wake lakini wameamua kufanya hivyo kwakupitia SACCOS kwa lengo la kuvutia wanachama wao, na kusisitiza kuwa riba zao nizachini zaidi kuliko zile zinazotolewa na mabenki

Hata hivyo, Bi Eunice ameeleza kuwa suala la (Universal Pension ) la kutoa pension kwa wazee ambao hawakuwa wanachama wa mfuko huo ni suala ambalo halitawezekana hivyo kuwataka wanachama wa mfuko huo kufikiria zaidi.

"Kumpa pensheni mzee ambaye hakuchangia kipindi ambacho alitakiwa kuchangia na baadae achukue kutoka kwetu sisi tuliochangia nisuala ambalo haliwezekani inatakiwa mliangalie kabla sheria hii haijapitishwa" Alisema Eunice 

Katika masuala ya kusaidia jamii NSSF bi. Eunice amesema kuwa kwa sasa shirika hilo linajikita zaidi katika kampeni za kutokomeza ugonjwa hatari wa maleria

"Kwa takwimu zilizotolewa na wizara ya afya hapa nchini, ugonjwa wa maleria ndio unao wauwa watanzania wengi hivyo na sisi lazima tuilinde jamii yetu katika magonjwa" amesema Eunice

Aidha, shirika hilo linatarajia kukusanya mapato ya shilingi Bilioni 181.1 kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kutoka kwenye vitega uchumi vyake ukilinganisha na mapato yaliyokusanywa ya shilingi Billioni 120.1 katika mwaka fedha uliopita 2012/2013.

 EJENZI WA VITUO VIPYA VYA MABASI YAENDAYO MIKOANI NA NCHI JIRANI

Halmashauri ya jiji la Dar es salaam inatarajia kujenga vituo vya mabasi katika maeneo ya Mbezi Luis, Boko Basihaya na Mbagala- Kongowe ikiwa ni vituo vya mabasi yaendao mikoani na nchi jirani kwa lengo la kuimarisha huduma za usafiri hapa nchini.    

Akizungumza na Blog hii mapema leo msemaji wa jiji hilo bwana Gaston Mwakwembe amesema, kituo cha mabasi Ubungo kitatumika katika mradi wa mabasi yaendayo kasi baada ya mradi huo kukamilika ifikapo mwaka 2014/2016, na kuwataka wakazi wa jiji hilo kutumia kituo cha ubungo huku ujenzi wa vituo hivyo vipya ukiendelea.

Hata hivyo Hot mix imefanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa jijini la Dar es salaam juu ya mpangilio wa vituo hivyo ambapo walikuwa na mtazamo tofauti.

Serikali imedhamiria kuondoa kero ya muda mrefu ya msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam, ambayo inaipotezea serikali mabilioni ya fedha, Hivyo kukamilika kwa miradi hiyo mitatu itaongezea serikali kipato na wananchi kwa ujumla.


EmoticonEmoticon