Wizara ya mambo ya ndani ya nchi Tanzania imetangaza kuanza
rasmi kwa zoezi la kuwaondoa wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia na
kuishi nchini kinyume cha sheria.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa mambo ya
ndani ya nchi Dkt Emmanuel Nchimbi wakati akiongea na waandishi wa habari,
ambapo Waziri huyo amesema kutekelezwa kwa zoezi hilo kunatokana na maelekezo
kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.
“Rais tayari amekamilisha kazi yake imebaki ya waziri wa mambo
ya ndani, hivyo na mimi nasema kuwa nitaanza kazi yangu ila sitawapa taarifa
nilini kikubwa nikuwa watoke hapa nchini kwetu na wasivunje sheria” alisema Nchimbi
Aidha waziri huyo hakuweza kutaja muda rasmi wa kuanza
utekelezwaji wa zoezi hilo na kufafanua kuwa litakuwa zoezi la kushtukiza
ambapo amewataka wahamiaji wote haramu waliopo nchini kuanza kurudi kwao haraka
iwezekanavyo kabla ya kuanza kwa zoezi hilo.
Jeshi la taifa, usalama wa taifa wanasubiri kauli ya kuanza kwa
zoezi hilo ambalo tutalitekeleza kwa kasi ya hajabu, nakuongeza kuwa viongozi
wa kijiji nao wasiwaruhusu au kuwaficha wasio watanzania hapa nchi. Amesema Nchimbi
NHC KUJENGA MAJENGO 3 DAR, YAGARIMU BILIONI 123 AJIRA ELFU 3
KUPATIKANA
Watanzania wametakiwa kutumia ardhi kwa ajili ya makazi bila
kusahau suala la maeneo ya mashamba ya kilimo ili kuendeleza uchumi pamoja na
upatikanaji wa chakula hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa
Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh. GoodLuck Ole Medeye, wakati wa
makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa majengo ya biashara na makazi jijini hapa
Katika makabidhiano hayo Naibu waziri amesema iwapo wakandarasi
waliokabidhiwa tender hiyo watachelewa gharama zitaongezeka hivyo itawalazimu
kutumia pesa zao wenyewe na amewataka kukamilisha kazi kwa wakati.
Zaidi ya shilingi bilioni 123 zitatumika katika mradi wa ujenzi
wa nyumba za makazi na biashara jijini Dar es Salaam katika mradi unaoendeshwa
na shirika la nyumba la taifa, mradi ambao utakamilika baada ya miaka miwili na
nusu ikiwa na lengo la kuweka makazi ya kisasa.
Mradi huo pia utaweza kuajiri watanzania zaidi ya Elfu 3 na
kuongeza majengo ya kibiashara pamoja na nyumba zaidi ya 520, Mkurugenzi wa
ubunifu wa shirika la nyumba la Taifa NHC amesema majengo hayo yatajengwa
katika maeneo ya Kinondoni- Hananasif, Upanga na Victoria jijin Dar es salaam.
Miradi hiyo mitatu ya nyumba za makazi na majengo ya biashara
imegawanywa katika muda tofauti mpaka kukamilika kwake, mkubwa zaidi utachukua
miezi 30 kukamilika na mdogo utachukua miezi 18 kukamilika na nyumba hizi
zitauzwa kwa watanzania.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi Tanzania imetangaza kuanza
rasmi kwa zoezi la kuwaondoa wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia na
kuishi nchini kinyume cha sheria.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa mambo ya
ndani ya nchi Dkt Emmanuel Nchimbi wakati akiongea na waandishi wa habari,
ambapo Waziri huyo amesema kutekelezwa kwa zoezi hilo kunatokana na maelekezo
kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.
“Rais tayari amekamilisha kazi yake imebaki ya waziri wa mambo
ya ndani, hivyo na mimi nasema kuwa nitaanza kazi yangu ila sitawapa taarifa
nilini kikubwa nikuwa watoke hapa nchini kwetu na wasivunje sheria” alisema Nchimbi
Aidha waziri huyo hakuweza kutaja muda rasmi wa kuanza
utekelezwaji wa zoezi hilo na kufafanua kuwa litakuwa zoezi la kushtukiza
ambapo amewataka wahamiaji wote haramu waliopo nchini kuanza kurudi kwao haraka
iwezekanavyo kabla ya kuanza kwa zoezi hilo.
EmoticonEmoticon