MCHAKATO WA KATIBA MPYA: AZAKI YALIA NA USHIRIKI WA WANANCHI BUNGE LA KATIBA, WAOMBA KURA YA MAONI IFANYIKE KATIKATI YA WIKI



Wakati rasimu ya pili ya katiba mpya ikisubiriwa kwa hamu na wananchi pamoja na wadau mbalimbali ili bunge la katiba liweze kuundwa kwa ajili ya kujadili rasimu ya katiba hiyo,




 Asasi za kiraia zaidi ya 37 zimeendelea kulia na idadi ya ushiriki wa wananchi katika mchakato huo kwa kuhofia idadi ya Wabunge ambao watahitaji kuunda Bunge la katiba.


Akitoa maazimio mbele ya wanahabari hii leo jijini Dar es salaam, juu ya Sheria ya marekebisho ya katiba sura namba 83, Bunge maalum la katiba, kura ya maamuzi au maoni. Tume ya marekebisho ya katiba pamoja na maudhui ya katiba hiyo.

Mwakilishi wa AZAKI ambaye ni Mkurugenzi wa TGNP bi. Usu Malya amesema siku ambayo kura ya maoni itapigwa isiwe Jumamosi, jumapili au ijumaa na badala yake iwe siku ya kazi pia matokeo yakiwa zaidi ya 50% basi katiba hiyo itakuwa imepita na chini ya Asilimia hizo katiba hiyo itakuwa imekataliwa


“Siku za ibada itaweza kuwanyima fursa wananchi wengi na haki ya kuabudu ila tukipiga kura siku ua kazi itatoa fursa kwa wananchi wote kushiriki kama ambavyo tunajumuika pamoja katika siku za sherehe mbalimbali zikiangukia katikati ya wiki” Alisisitiza Bi. Usu Malya


Bi. Usu amesema nivyema kuandaliwe vifaa maalumu vitakavyo tumiwa na makundi maalum kama walemavu ilikuwapa fursa watu wote kutoa maoni yao, pia uwakilishi wa asasi za kirai, vyama vya kutetea makundi maalum, wanaharakati nao wapewe nafasi ya usawa ilikuweza kutoa maoni yao katika Bunge lijalo


Aidha mwanasheria wa kituo cha sheria na haki za binadamu bwana Arold Sungusia amesema wao wamekuwa wakitoa maangalizo mbalimbali juu ya vitu vinavyo endelea hivyo ni vyema kwa serikali na jamii kuamua kutekeleza kwani tayari wametoa maangalizo mbalimbali juu ya mchakato huu wa katiba mpya


Katika suala la raslimali za taifa ambazo ni ardhi, madini,gesi na Mafuta AZAKI imesema ni vyema katiba mpya izingatie Azimio no.1803 la mwaka 1962 juu ya umiliki wa milele wa raslimali wa nchi wanachama wa umoja wa mataifa


Mchakato wa katiba kwa sasa umebakiza hatua tatu ili kukamilika ingawa mpaka sasa Rasimu ya pili ya katiba mpya bado haijakamilika, hatua hizo ni Kutolewa kwa rasimu ya pili, Bunge la Katiba pamoja na Kura ya maoni ambayo itaruhusu kupitishwa kwa katiba hiyo au kutopitishwa kwa kwa katiba hiyo.


EmoticonEmoticon