Tanzania kukaa giza kwa siku 10 bila umeme

Shirika la umeme nchini Tanzania Tanesco limetangaza kuwepo kwa umeme wa mgao kuanzia tarehe16 mpaka 26 mwezi huu kutokana na upungufu wa gesi katika kisiwa cha songosongo kilichopo wilayani Kilwa kuwa na matengenezo ya kiufundi
Shirika hilo linategemea kisiwa hicho kupata gesi ya kuzalishia umeme ambapo vituo vya kuzalisha umeme kama Ubungo, IPTL na nyingine zinazo zalisha umeme kwa kiwango kikubwa zitaadhiriwa na ukosefu huo hivyo kupelekea kuwepo kwa mgao huo

Akiongea katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es salaam, msemaji wa shirika hilo bi Badra Masoud amesema matengenezo hayo ni muhimu na haya kwepeki hivyo ndani ya siku 10 kuanzia kesho mgao wa umeme utaanza.
“Mgao huu utakuwa wa muda si kwamba umeme hautakuwepo kabisaa, kama mnavyo jua hivi sasa tumepunguza uzalishaji wa vyanzo vya maji kutokana na mabadiliko ya Tabia nchini na tunategema sana Gesi hivyo tutakosa gesi kutoka songosngo” Alisema Badra.

Kutokana na matengenezo hayo mikoa iliyo unganishwa katika gridi ya taifa ndiyo itaadhirika kwa kukosa umeme, mikoa hiyo ni Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Dodoma, Pwani, Singida, Tabora, Manyara, Mara, Morogoro pamoja na Zanzibar.

Mikoa ambayo aitaadhirika na mgao huo niile ambayo haijaunganishwa kwenye gridi ya taifa nayo ni Ruvuma, Rukwa, Mtwara na Lindi.

Siku chache tu Bi Badra akiwa kikaangano live kupitia ukursa wa facebook w a kituo cha utangazaji EATV Bi. Badra alisema hakuta kuwa na mgao wa umeme nakuwa kilicho kuwa kina endeleo mpaka kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo ni matengenezo madogo madogo yaliyo kuwa yakifanywa na shirika hilo

Katika kipindi hicho bi Bandra alisema watanzania hawataki maneno yakuwa umeme upo na badala yake wanataka umeme nakuhidi kuwa shirika hilo litawapa huduma ya umeme
Hata hivyo uongozi wa Tanesco unaomba radhi kwa usumbufu utaokao jitokeza kwa baadhi ya maeneo yatakayo kosa umeme

Ikumbukwe kuwa shirika hilo limetuma maoni yake ya kupandisha bei za umeme ifikapo mwakani licha ya kutoa huduma isiyo ridhisha kwa wateja wake.


EmoticonEmoticon