DKT. GHARIB BILAL “UKIWA NA VIRUSI VYA UKIMWI USIWAAMBUKIZE WENGINE”

 
Wananchi wametakiwa kutowaa mbukiza wengine virusi vya ukimwi, Wajikinga na maambukizi mapya pamoja na kuwa na uelewa wa ugonjwa wa ukimwi ili kupunguza madhara ya gonjwa hilo hapa nchini



Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akivishwa Beji ya kupiga vita dhidi ya Virusi vya ukimwi katika wiki hii ya kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani na Viongozi wa Umoja wa vijana CCM jijini Dar es salaam.

Dkt Gharib Bilal amesema taifa lolote lenye maendeleo ni lile ambalo wananchi wake wana afya njema, uelewa mkubwa juu ya afya zao kwani wananchi wakiwa na afya duni shuguli za maendeleo zinarudi nyuma.

Watu wengi wanauelewa juu ya ugongwa wa Ukimwi lakini hatuwezi kuacha bila kuwaambia mara kwa mara, kupima afya yako nimuhimu ujue kama umeambukizwa ili uishi kwanjia salama na kama hujaambukizwa pia ujikinge usiambukizwe hivyo waliobainika kuwa na VVU wasiambukize wengine ilituwe na jamii yenya Afya njema.

“Ni lazima tuwaambie mara kwa mara juu ya “NO 3 hakuna maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi, hakuna Vifo vya ugonjwa wa ukimwi, hakuna unyanyapaa kwa wagonjwa wa ukimwi” Amesema Dkt Gharib Bilal

Dkt Bilal amesema kwa karne zijazo bara la Afrika ndilo litakuwa na nguvu kazi kubwa duniani ambao ni vijana hivyo ni vyema kuanza kuwaandaa kwa njia mbali mbali ikiwemo kuweka usalama wa afya zao

“Vijana ndio wahanga wakubwa wa gonjwa hili kwani wao wana mihemko kuliko wazee hivyo kuwapa elimu kila mara kutajenga akili yao kujali kupima, kutoambukiza wengine ili baadae tuwena nguvu kazi kubwa katika nchi yetu na bara la Afrika kwa ujumla” Amesema Dkt Gharib Bilal

Aidha Dkt Gharib Bilal amewapongeza viongozi wa UVCCM kwakujali afya za vijana kwani bila kufanya hivyo watapoteza nguvu ya taifa ambao wao wanawajibika kwao.

Naye Katibu wa hamasa na chipukizi wa UVCCM Taifa bwana Poul Makonda amesema wanatambua mchango wa vijana katika kuendeleza taifa hivyo na ndio maana wameamua kumshirikisha Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal kuwasaidia katika kuhakikisha kuwa afya za vijana wa Tanzania zinakuwa salama

Bwana Poul Makonda amesema siku ya maadhimisho ya Ukimwi duniani watatoa huduma za vipimo vya magojwa mbalimbali ikiwemo Virusi vya Ukimwi katika Viwanja vya Biafra- Kinondoni jijini Dar es salaam huduma ambazo zitakuwa bure bila malipo yoyote

“Nawataka vijana wajitokeze pale Biafra siku ya Ukimwi Duniani, tutawapa fursa ya kupima magonjwa mengi sana ikiwemo VVU, Kansa ya Titi, Presha na magonjwa mengine na hii ni bure kwa ajili yao kwani tuna wadhamini sana vijana”Asema Makonda

Viongozi wa Kitaifa wa umoja wa vijana CCM - UVCCM toka maeneo mbali mbali hapa nchini watajitokeza siku hiyo kuhakikisha kuwa wana kamilisha usalama wa Afya za vijana wajumbe hao ni pamoja na Daudi Ismail ambaye ni mjumbe wa NEC Pemba, Amani Kajuna ambaye ni Mwenyekiti wa vijana Mkoa wa Mbeya, Bwana Yahaya Mwenyekiti wa UVCCM – Kagera pamoja na Salma Mohamed UVCCM Tanga.

Kila tarehe Moja ya mwezi wa 12 kila mwaka Dunia inaadhimisha vita dhidi ya Virusi na Ugonjwa wa ukimwi hivyo UVCCM wameamua kumvisha makamu wa rais jukumu la kushugulikia tatizo hilo kuelekea kilele cha siku hiyo.


EmoticonEmoticon