P-SQUARE WAAHIDI SHOO YA NGUVU BONGO, NI MWENDO WA PESONALITY

Kundi la P-SQUARE lililotua jana nchini Tanzania toka Nigeria kwa ajili ya tamasha kubwa litakalofanyika siku ya kesho pale Leaders club wameahidi kutoa burudani yenye kiwango cha juu kwa watanzania wote watakaohudhuria.


Wasanii hao mapacha kesho jukwaani watapiga muziki wa LIVE na bendi kwa mfululizo wa masaa zaidi ya mawili huku wakipewa shavu na Lady Jay Dee, Professa Jay, Joh Makini na Ben Pol.

Tamasha hilo kubwa la muziki kwa mwaka huu, linatarajiwa kuanza saa 1 jioni bila kuchelewa.


EmoticonEmoticon