Mwili wa askari aliyeuawa kwa kupigwa
risasi Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC Afisa Luteni Ahmad Rajab
Mlima umeagwa na kuzikwa leo katika makaburi ya kisutu jijini Dar Es
Salaam.
Mwili huo uliagwa katika kambi ya Jeshi
la Wananchi wa Tanzania la Lugalo ambapo heshma za kijeshi zilitolewa
kisha mwili huo kupelekwa nyumbani kwao Mbezi Beach kwaajili ya
kuagwa na familia kisha kupelekwa katika makaburi ya Kisutu kwa
maziko.
Akisoma Risala kwa niaba ya mkuu wa
majeshi ya ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, wakati wa
shughuli ya kuagwa kwa askari huyo, Mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni
Jenerali Samwel Albert Ndomba amesema, Luteni Mlima alikumbwa na
umauti wakati akilinda amani katika mji wa kiwanja uliopo mpakani mwa
DRC, Rwanda na Uganda.
Luteni General Samwel amesema, Marehemu
alikuwa na wenzake katika shuguliza kulinda amani ndipo alipigwa
risasi na watu ambao hakuwataja siku ya Jumapili tarehe 27 nakufariki
hapo hapo. Alisema Luteni General Samwel
Aidha mgeni rasmi
katika shughuli hiyo, Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mh.
Shamsi Vuai Nahodha amesema, pamoja na kumpoteza Luteni Ahmad, bado
Jeshi la Tanzania litaendelea na Operesheni ya amani nchini DRC,
nakuhakikisha kuwa amani inakuwepo nchini humo
Naye kaka wa
marehemu Dr. Aziz Mlima ametoa shukrani kwa jeshi la Tanzania na
jeshi kwa ujumla kwa kushiriki katika msiba wa ndugu yake.ambapo
marehemu ameacha mtoto mmoja na mchumba ambaye walitarajia kufunga
ndoa Dec. mwaka huu.
Huyu ni mwanajeshi
wa 3 wa Tanzania kuuwawa ndani ya mwaka huu tangu Majeshi ya Tanzania
kupeleka majeshi yake nchini humo.Hatahivyo mapambano yanaendelea
ambapo hivi sasa majeshi ya serikali yamefanikiwa kuteka ngome ya M23
huko Goma ambapo mkuu wa jeshi la waasi amekimbiliwa nchini Uganda.
EmoticonEmoticon