SHIRIKISHO LA KISIASA LA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI, TANZANIA YATAKA WANANCHI KUKUBALI


Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa haitokubali kushiriki mpango wowote wa kuharakisha uundwaji wa shirikisho la kisiasa la nchi za Afrika Mashariki pasipo ridhaa ya wananchi wake.

Taarifa kutoka ndani ya wizara ya Afrika Mashariki zimesema,


Hatua hiyo ya Tanzania inatokana na mpango unaoendeshwa hivi sasa na nchi za Rwanda, Kenya na Uganda wa kutaka kuundwa kwa shirikisho hilo ifikapo mwaka 2015.

Taarifa ya waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania mhe. Samuel Sitta inayosema kuwa itashangaza sana iwapo shirikisho litakaloundwa pasipo ridhaa ya wananchi na kuwa itakuwa ngumu kwa shirikisho hilo kudumu, kutokana na mifano mingi kama nchi za Misri, Syria na Libya kushindwa kuunda shirikisho hilo.


Kauli hiyo ya Tanzania imekuja kipindi ambapo jumuiya ya Afrika Mashariki imekamilisha rasimu ya umoja wa fedha, hatua muhimu ya mwisho kabla ya kuundwa kwa shirikisho la kisiasa ambalo kwa mujibu wa ratiba iliyopo, shirikisho hilo linatakiwa liwe tayari ifikapo mwaka 2015.

                      BENKI YA DUNIA YATABIRI KUPOROMOKA KWA UCHUMI

Magavana wa benki ya dunia wametoa tamko linaloeleza kuto ridhishwa na mwelekeo wa kiuchumi duniani na madhara yake kwa mataifa maskini duniani ikiwemo Tanzania.

Tamko hilo limekuja baada ya mkutano wao uliofanyika jijini Washington Marekani na taarifa yake kupatikana jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, wametaka nchi tajiri zitambue madhara ya sera zao kwa uchumi wa dunia na hatua zinazofaa kuchukuliwa katika kukabiliana na kuporomoka kwa uchumi.

Kwa mujibu wa tamko hilo, magavana hao wametaja madhara yanayotokana na matokeo mabaya ya kiuchumi kuwa ni kukosekana kwa fedha za bajeti za maendeleo, kuporomoka kwa bei za bidhaa na kushuka kwa kiwango cha biashara baina ya nchi na nchi.


EmoticonEmoticon