Serikali imeshauriwa kuongeza
kodi katika bidhaa za samani zinazoingizwa hapa nchini ili kuweza
kuongeza dhamani ya soko la samani zinazo tengenezwa hapa nchini na
kuwawezesha wabunifu wa ndani kujiongezea kipato.
Akiongea katika mahafali ya
kuhitimu kwa wanafunzi wa chuo cha ufundi cha Mtakatifu Gasper pamoja
na wanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiy Mkuu wa chuo hicho
Padri Achileus Mutalemwa amesema kuwa ni vyema serikali ikatambua
kuwa samani kutoka nje ni chanaga moto kubwa kwa watanzania wao
jishugulisha na fani hiyo.
“Kwa bidhaa za samani zinazo
agizwa nje endapo serikali ingeoweka kodi kubwa ingewezesha wauzaji
wa ndani kuwa na faida lakini kodi yao nisawa na kodi za wauzaji wa
ndani jambo linalopunguza ushindani wa kibiashara na kipato”
alisema Padri Mutalemwa
Baadhi ya wanafunzi ambao
wanasoma masomo ya ufundi wame waasa wanafunzi wenzao kupenda masomo
ya juwawezesha kujiajiri mara tu wamalizapo masomo yao pamoja na kuwa
wabunifu
Wanafunzi hao ni Tumainieli
Makundi ambaye alionyesha uwezo katika kutengeneza sofa, kabati na
meza huku mwenzake Adson Bang akionyesha umahiri katika kutengeneza
meza ambayo pia inatumika kama mbuzi ya kukunia nazi.
Shule ya mtakatifu Gasper kwa
ngazi ya chuo ilianzishwa mwaka 1988 kwa lengo la kutatua tatizo la
ukosefu wa ajira kwa kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kujitegemea, na
kwa upande wa shule ya sekondari ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa chini
ya taasisi ya kidini.
EmoticonEmoticon