MCHAKATO WA KATIBA MPYA: JK,LIPUMBA,MBATIA NA MBOWE WAJADILI IKULU


 
KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa leo, Jumanne, Oktoba 15, 2013 ameanza kukutana na viongozi wa siasa vyenye Uwakilishi Bungeni kujadili maendeleo ya mchakato wa Katiba Mpya nchini.

Viongozi wanaoendelea kukutana na Mheshimiwa Rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam sasa katika mazingira maelewano na mwafaka, ni Mwenyekiti wa Chama cha CUF Mheshimiwa Ibrahim Lipumba ambaye ndiye msemaji wa viongozi hao, Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mheshimiwa James Mbatia.

Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Philip Mangula, Mheshimiwa Isaack Cheyo ambaye anamwakilisha Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mheshimiwa John Cheyo na Mheshimiwa Mrindoko ambaye anamwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mheshimiwa Augustine Mrema. Waheshimiwa John Cheyo na Mrema wako nje ya nchi.

Pamoja na viongozi hao pia yuko Mheshimiwa H. Mnyaana Bwana Julius Mtatiro wa Chama cha CUF, Waheshimiwa Tundu Lissu na John Mnyika wa CHADEMA na Bwana Martin Mng’ongowa NCCR - Mageuzi.

Viongozi hao wamekutata kujadili juu ya mvutano uliopo juu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kikwete kusaini muswada wa sheria wa marekebisho ya sheria ya katiba mpya. kwani kusainiwa kwa sheria hiyo kutapele mambo mbali mbali ambayo hayaja fanyiwa marekebisho kupitishwa.


EmoticonEmoticon