CHUO CHA HESABU KUANZISHWA HAPA NCHINI


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa hapo jana amekutana na kufanya 
mazungumzo na Wajumbe wa African Institute for Mathematical Sciences – Next Einstein Initiative kuhusu kuanzishwa kwa Chuo cha AIMS - NEI hapa Tanzania.

Wajumbe hao walimtembelea Waziri Kawambwa ofisini kwake  kufuatilia kunzishwa kwa  chuo hicho hapa nchini.  Waziri Kawambwa ameuhakikishia ujumbe huo kuwa Serikali ya Tanzania itatekeleza kikamilifu  wajibu wake katika mchakato wa  kuanzisha chuo hicho.

Picha hapo juu ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa  (wa kwanza kulia), akiwa katika mazungumzo na Wajumbe wa African Institute for Mathematical Sciences (AIMS) – Next Einstein Initiative (NEI), Samuel Awuku Chief Operating Officer, AIMS - Tanzania  (Wa pili kutoka kulia), Julie Staples Diector, Organisational Learning and Oversight, Profesa Estomih Masawe Balozi wa AIMS - NEI, Tanzania na wa kwanza kushoto ni Paulina Mkoma, Afisa - Idara ya Elimu ya Juu, Wizara ya  Elimu na Mafunzo ya Ufundi. 


EmoticonEmoticon