Wananchi
zaidi ya 40,000 wa vijiji 30 katika wilaya za Arumeru na Longido
mkoani Arusha wanakabiliwa na tatizo kubwa la kukosekana kwa maji
katika maeneo yao kutokana na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji
unaoendelea katika maeneo yao
Vyavyo
vya maji vilivyo adhirika katika chemchem zinazotoka katika msitu wa
mlima Meru huku serikali ikiombwa kuchukua hatua za haraka
kukabiliana na tatizo hilo.
Uharibifu
huo umefanyika katika kata ya ngarananyiki ambapo wananchi na
viongozi wa kata hiyo wamesema pamoja na kufanya jitihada za
kudhibiti tatizo hilo bado linaendelea nakuomba serikali katika ngazi
za juu kuliangalia suala hilo kabla madhara hayajawa makubwa
Wananchi
waliotoa ombi hilo ni pamoja na Julius Ayo, Furaha Mungure na Barnaba
Simon, ambapo wamesisitiza kuwa kuharibiwa kwa vyanzo hivyo ndio
chanzo cha hatari ya kukosekana kwa maji safi na salama katika maeneo
yao
Aidha
baadhi ya viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali wakiwemo wale
wakutoka katika kamati ya mazingira wametembelea eneo hilo na
kujionea hali halisi na kuahidi kufikisha suala hilo katika ngazi ya
mkoa
Viongozi
hao ni Bwana Onesmo Nangole ambaye ni mwenye kiti wa mkoa wa Arusha
kwa tiketi ya chama cha CCM.
EmoticonEmoticon