WAMILIKI WA MABASI DAR WATAKIWA KIJIPANGA KIBIASHARA

Chama cha wamiliki wa Mabasi jijini Dar es Salaam, kime waasa wamiliki wa mabasi kuwa tayari kwaajili ya changa moto za kibiashara zitakazo letwa na mradi wa mabasi yaendayo kasi


M/Kiti wa chama hicho Bwana Sabri Mbabruk amesema biashara za Mabasi azitaendeshwa tena na mtu mmoja mmoja na badala yake kutakuwa na kampuni mbili tu kwaajili ya kufanya biashara hiyo

Aidha amesema kuwa ilikupunguza msongamano wa magari jijini, serikali imeamua kubadili mfumo wa uendeshaji magari jijini na kuazimia kuanzisha mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.

kwa upande mwingine, mamlaka ua udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA, itasitisha utoaji leseni kwa wamiliki wa daladala, na kusitisha swala la kurudia leseni ifikapo juni mwakani.Nakuwa taka wamiliki wa barabara ya Kilwa na Alhassan Mwinyi kuanza kuunda makundi yao.


EmoticonEmoticon