UGANDA KUSHUGULIKIA MAKAMPUNI YA SIMU
Serikali ya Uganda imetangaza kuyatoza faini makampuni ya simu yatakayo kuwa na matatizo katika mawasiliano

Tume ya mawasiliano ya nchi hiyo, imesema tayari imeunda chombo maalum chenye mfumo wa computer utakayo fuatilia mitandao itakayo kuwa na matatizo kama vile simu kukata mawasiliano, kukatika, makampuni kutoza viwango zaidi ya zile inavyotangaza.

kwa mujibu wa mkurugenzi wa mawasiliano ya kisheria wa Tume ya Mawasiliano nchini humo UCC Susan Wegoye, amesema faini hizo zitakuwa zikiangalia nikiasi gani cha hasara ambacho kampuni husika imesababisha kwa watumiaji wake kwa muda wa mwaka mzima

pia amesema faini azitatozwa endapo tu,matatizo hayo ya kimtandao yatakuwa yamesababishwa na majanga yasiyo weza kuzuilika kama vile mafuriko,dhoruba na vita.


EmoticonEmoticon