FASHION&BEAUTY

 PEPLUM - VAZI LINALOPENDEZA SANA KINADADA HATA WASIO NA UMBO ZURI

 
  

Peplum, ni vazi linalo pendwa na kinadada wotehasa wale wanaotoka nchi za Ulaya lakini hizi sasa imekamata hata anga za mitindo nchini,

 kutokana na nakuwa hawana maumbo mazuri sana. vazi hili linampendeza kila mtu mwenye umbo zuri au asio na umbo zuri


Vazi hili, ni miongoni mwa sataili ya mavazi ya kizamani enzi za 80, lakini zimerudi tena kwenye Fashion na lakini kwa kuboreshwa zaidi kiasi cha kila mtu kuvutiwa na vazi hili

Aina hii ya mavazi humpendeza kila mtu, na kwamwaka 2013 katika ulimwengu wa mitindo vazi hili limeibuka zaidi.

Kuna aina mbalimbali ya vazi hili, kuna viplauzi, Gauni na Sketi lakini unashauriwa kuwa nimuhimu kushona Peplum ambayo niyamabega wazi kutokana na staili yake ya kumwaga hapo katikati ili kuleta mvuto zaidi 

 *****************************************

 FLAVIAN MATATA MWANAMITINDO BORA MWAKA 2012 BARANI AFRIKA


Mwanamitindo Flavian Matata ambaye anang’ara katika Ulimwengu wa Kimataifa hivi sasa, amezidi kung’ara baada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super Model na kuwa mwanamitindo bora barani Afrika kwa mwaka 2012( Africa’s Most Outstanding Model 2012)

 

Tuzo hiyo imemuangukia Flavian, kwa kuwa mwanamitindo ambae anailetea sifa Afrika katika anga za Kimataifa. Mwaka jana Flaviana alipokea tuzo nyingi kutoka kwa wanamitindo wa Barani Afrika kituambacho kimempa nafasi nzuri ya kushinda na kuwa bora zaidi

Kwa sasa Flavian anaishi Nchini Marekani katika jiji la New York, akifanya shuguli za mitindo kupitia shirika la Wilhelmina Models, Flavian ameweza kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na umahiri wake katika maonyesho ya mavazi
Mwaka 2007

Flavian Matata alitwaa taji la Miss Universe Tanzania , ambapo alifanikiwa kufika katika nafasi ya sita katika mashindano ya Kimataifa ya Miss Universe.



 ****************************************

EMERALD NDIO RANGI YA MWAKA 2013 

        colour of the year 2013- emerado-pantone



Kwa kawaida wataalamu wa urembo hutoa rangi ambayo inatawala kwa mwaka huo ambapo mwaka huu ni Emerald- Pantone

mwakajana 2012 rangi ilikuwa Tangerine Tango, 2011 Honeysuckle, 2010 Turquoise, 2009 Mimosa, 2008 Blue Iris na 2007 ilikuwa ni Chilipapper

 

Posted on: Jan.8.2013

By: Loyce Joseph 

****************************************

MREMBO JOSELYNE MARO ANASTAHILI TAJI LA MISS EAST AFRICA 2012

JOSELYNE MARO KATIKATI AKIWA NA WASHINDI NO.2 NA 3
JOSELYNE AKIFURAHIA USHINDI WAKE


Tanzania sasa imeacha kuwa msindikizaji katika mashindano ya Miss East Africa, baada ya Mrembo Jocelyne Maro kunyakuwa taji hilo, tangu mashindano hayo yalipo anzishwa.

Jocelyne alizawadiwa Dola Milioni 30.000, pamoja na Gari aina ya Toyota Verosa.  

.................................................................................

MISS USA. OLIVA CULPO AIBUKA MISS UNIVERSE 2012, AWABWAGA WENGINE 89

Miss Universe 2012,akivishwa taji na Miss Universe 2011





Olivia Culpo, Miss USA, ndiye ameibuka na kutwaa taji hilo la Miss Universe 2012, Olivia ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Boston marekani anaumri wa miaka 20, na nimmarekani wa nane8 kutwaa taji hilo, tangu miaka 15 iliyopita kwa taifa hilo kushinda

MISS UNIVERSE 2012 AKIFURAHIA TAJI HILO

Hali sio nzuri kwa Miss Universe Tanzania, Baada ya mshiriki huo kuwekwa miongoni mwa waliofeli, Winfrida Dominic



MISS UNIVERSE TANZANIA 2012
 
Tuliwakilishwa na Winfrida Dominic, mrembo kutoka tanzania ambaye alishinda nafasi ya Miss Universe Tanzania 2012, amepata nafasi nzuri katika Mashindano mengine, lakini akufanikiwa kufanya vizuri katika mashindano yaliyofanyika taree 19.

 .............................................................................................................

  WINFRIDA DOMINIC MISS UNIVERSE TANZANIA 2012 KATIKA POZI TOFAUTI


WINFRIDA NIMIONGONI MWA WAREMBO KIBAO WATAKAO PANDA JUKWAANI KUWAKILISHA NCHI ZAO KATIKA MASHINDANO YA MISS UNIVERSE YANAYO FANYIKA HUKO LAS VEGAS NEVADA LEO TAREHE 19.12.2012

TADA EDWARD ANAWAKILISHA Set. Lucia
Picha ya pamoja ya Miss Universe wote
.................................................................................

NADIA NIMEKUWA ZAIDI KIMITINDO BAADA YA KUIBUKA, THE BEST FEMALE MODEL OF THE YEAR 2012

Nadia, ambaye ameibuka kuwa best Female Model of the Year, katika kinyang'anyiro kilicho fanywa na Swahili Fashion Week, iliyofanyika jijini Dar es salaam, Amesema kuwa kupewa nafasi hiyo nikuonyesha jinsi gani amekuwa katika tasnia ya mitindo nchini na kuwa shukuru sana mashabiki kwa kuona anachokifanya katika majukwaa ya Urembo

NADIA AHMED, aliuambia mtandao wa Cumpas Vision kuwa, Nafasi aliyopata imemfanya ajue kuwa yeye sio Model tu, ila nimiongoni mwa wanaofanya vizuri ndani ya Mitindo hapa nchini









"Nimepata kujua kuwa watu wanatambua na kupenda ninacho kifanya, pia nimeona kazi yangu kwa miaka 3 sasa, tangu nianze kushiriki Runways tofauti tofauti, nimefurahi sana" alisema Nadia









Nadia aliongeza kuwa, kwa sasa amepata kujua nijinsi gani Disigner mbali mbali wanadhamini mchango wake, pindi anapo watanzazia mavazi yao.

Nadia ameibuka kuwa Best Female Model of The Year katika Tuzo iliyoandaliwa na kutolewa na Swahili Fashion Week iliyo malizika wiki mbili zilizo pita jijini Dar es Salaa

...................................................................................

MISS TANZANIA 2012,BRIGITA ALFRED KATIKA PICHA NA WANAFUNZI WA SHULE YA WALEMAVU YA MUGEZA MSETO HUKO BUKOBA, BAADA YA KUWAPA MSAADA WA VITU MBALIMBALI

   .......................................................................

NGOMA MPYA YA ZUHURA YAZIDI KUTAMBA


Aliyekuwa Miss face of Afrika Tanzania 2006, Zuhura Mrisho, ametoa ngoma yake Mpya inayokwenda kwa jina la "Mazoea" ngoma hiyo ambayo inatamba hivi sasa itakuwa miongoni mwa nyimbo nyingine 8 ambazo zipo kwenye Album yake ya pili.
 

Ngoma hiyo ya Mazoea,imemtambulisha kivingine Star huyo, kwa staili tofauti na yazamani aliyotumia kwenye Album hiyo, Aina ya muziki alio tumia Zuhura kwenye Album hii ni miondoko ya Zuku na Raga, ikiwa pamoja na miondoko ya kiafrika zaidi.
 
"Mashabiki wangu walizoea miondoko ya kisukuma ambayo nilitumia kwenye Album ya kwanza, hivi sasa wataniona kwenye staili nyingine, nimefanya hivyo ilikuwa furahisha mashabiki wangu pamoja na mabadiliko yaliyopo sasa kwenye tasnia ya Muziki"alisema Zuhura akiongea na Campus Vision 
 
Zuhura ambaye amejaliwa vipaji vingi sana. anaendelea vizuri na fani yake ya mitindo na kuwa yuko tayari kama atapata mtu wakumsimamia katika fani ya Mitindo ambayo nayo pia nimiongoni mwa mambo anayo fanya kwa kiwango cha juu.
 
Tayari zuhura ana Album moja iliyotamba sana kama Limupenzi ikiwa na nyimba 12 ndani yake, na wimbo ambao ulibeba Album hiyo ni "Limupenzi", iliyo sheeni miondoko ya kisukuma.Maandalizi ya Album ya pili yenye nyimbo 8 unaendelea vyema, na muda mfupi utawafikia mashabiki wake, alisema Zuhura
    ....................................................................

MAMBO MADOGO YENYE FAIDA KUBWA KWA AFYA YAKO KAMA UKIZINGATIA



        ..............................................................................................................................................

 NIRVANA YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK 2012

Kipindi cha mitindo kinacho rushwa na Station ya Kijanja EATV, inayotambulika kama Nirvana kimechaguliwa kuwa kipindi bora cha mitindo cha runinga katika tuzo za Swahili Fashion Week  iliyomalizika  jijini Dar es Salaam.


Nirvana imejinyakulia Tuzo hiyo Miongini mwa Vipindi vingi ambavyo vilikuwa vikiwania Tuzo hiyo, kipindi hicho kinacho ruka kila Jumanne saa 1 kamili usiku kupitia Ting'a Kali Namba Moja kwa vijana EATV na kinatangazwa na Lotus&Deo



Muandaaji wa Kipindi hicho Bhoke Egina na aliye waikuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Big Brother Afrika alitoa shukrani zake juu ya tuzo hiyo, alipokuwa akiongea na mtandao wa Cumpus Vision, huku akiwashukuru watanzania kwa kupigia kura kipindi hicho



Wabunifu mbalimbali,Models na wengine wengi wanao husika na Mitindo walipewa walicho stahili yani Tuzo na Swahili Fashion Weeek,akiwemo Martine Kadinda, Nancy Sumari na wengine wengi


  .........................................................................
NANCY SUMARI AWASHUKURU WATANZANIA,TUZO ZA SFW 2012
 Nancy Sumari ambaye ameshinda tuzo ya Swahili Fashion Week katika kipengele cha Stylish Female of the Year, amewashukuru watanzania na wale wote ambao walimpigia kura iliyopelekea yeye kushinda kinyang'anyiro hicho.


 Nancy,ambaye alikuwa Miss Tanzania.Nimiongomi mwa miss Tanzania wa zamani ambao wanafanya vizuri katika ulimwengu wa Mitindo ndani na nje ya nchi
................................................................

 YALIYO JIRI KATIKA SWAHILI FASHION WEEK,TAMADUNI ZA KIAFRIKA 

hizi ni baadhi ya picha za Models wakipita jukwaani kuonyesha mavazi ya wabunifu mbali mbali
maonyesho ya swahili fashion week yanafanyika jijini Dar es Salaa


picha kwa hisani ya www.misiepopular.blogspot.com
......................................................................  
 SWAHILI FASHION WEEK YAANZA LEO

Maonyesho ya mavazi ya Swahili Fashion Week, yameanza leo jijini Dar es Salaam. ikijumuisha Wabunifu mbalimbali wa nchini Tanzania pamoja na wabunifu kutoka katika nchi zingine barani Afrika.

Maonyesho ya Swahili Fashion Week, yanafanyika katika hoteli ya Golden Tulip.na Models kutoka tanzania watapewa kipaumbele katika Runway japokuwa kuna wengine kibao watapanda jukwaani

Swahili Fashion Week, imeweza kutangaza sanaa ya ubunifu nakukuza mavazi ya kiafrika katika ukanda wa Afrika na Dunian

.........................................................................
 Diamond Kama the late Michael Jackson
amelewa kweli
 
ukiangalia zaidi mavazi na mengine yanayo vutia macho katika matukio ambayo yatakuwepo katika Video ya NATAKA KULEWA, nikweli Diamond amelewa.
Rangi ambazo ametumia zina mvuto, zinaendana na maudhui ya wimbo, location ya club pia imetulia na kuleta mzuka zaidi, lakini kupiga vyombo mwenyewe kumeongeza mzuka sana na kalewa kweli na vyombo hivyo
Ma Dancer wa Diamond watakavyo tokelezea kwenye Video ya Nataka kulewa

Collar Neckless kuusika pale kati kama ambavyo mnamuona huyo mdada Nicole,katupia shingoni

........................................................................................................................................................................

 Sharo Milionea alikuwa mkali wa Swagga
Mareemu Sharo Milionea, jina kamili ni Husein Ramadhani. Muda wote Sharomilionea alikuwa ana muonekano na mvuto kutokana na jinsi alivyo jiwekea muonekano wake ambao ulikuwa unamfanya awe wakipeke
Ata kumbukwa kwa Style yake ya ya kuweka Bandage shavuni mithili ya NELLY wa majuu, Mikogo ya kutembea hata Mavazi yakuvutia na kumfanya mtu kumtazama kila wakati
 
Kauli za Kisharobaro, Oooh mama ....usinichafue Men, kamata mwiz menn...namengine kibao, alikuwa mcheshi asiye na makuu
 Sharo Milionea amefariki akiwa na miaka 26, kwa ajali ya Gari huko Mkoani tanga
.......................................................................................................................................................................


Collar Neckless, Huongeza Mvuto wa Muonekano

          Uvaaji wa cheni shingoni umekuwa ukiwapa wanawake wengi muonekano mvuri na mvuto maeneo ya shingoni, na hii nikwa wanaume pia. kuna aina ya cheni ambayo ndio iko sokoni kwa sasa na upendwa na wana wake wengi....Collar Neckless au Kola Cheni.


hii niyakuvaa shingoni

Kizuri kwa
aina hii ya kola ambayo inacheni unaweza kuvaa na aina tofauti tofauti ya nguo, cha msingi nikuhakikisha kuwa unaangalia mazingira ambayo yanafaa kwa mtoko wako kama ni mchana au usiku
Kizuri kwa aina hii ya Cheni, umpendeza kila mtu na aibagui rangi, cha muimu cha kuzingatia nipindi unapotaka kuvaa, angalia aina ipi itaendana na nguo zako, mahali unapo enda na wakati usika aidha ni usiku au mchana

..................................................................................................................................................... 
Miparo ya Mishell Obama, Aibagui Rika
kutokana na mvuto wa siasa za marekani, CampusV  inakupa tips za Fashio za mama Barack Obama Bi Mishel Obama, Je unajua mavazi na muonekano wake umekuwa kivutio kikubwa sana kwa kina dada,kina mama na hata wanawake watu wazima wa marekani na Dunia kwa Ujumla.
Mavazi yako yanaweza kukupa ushindi au kufanya watu wote wakugeukie, nakukuangalia kwa kila ufanyalo na hapa ndio ulimwengu wa fashion unapokuita fashionist au mwana mitindo   Mavazi yanamaanisha sana maisha yako kwa ujumla na mitazamo yako ambayo mtu hawezi kuona, kwajili hiyo kama wewe nimchafu au msafi utabainika tuu.
Watu wengu huofu kuusiana na rangi,lakini kadri fashion inavyo badilika akuna hofu tena ya rangi bali nikujua rangi hipi itakufaa kulingana na wakati unaotaka kutoka au unaenda katika mazingira gani na kwa nini,. Mishell Obama amekuwa mother of the Moth kwa mavazi na muonekano wake.


EmoticonEmoticon