Imebainishwa kuwa kufanyabiashara kwa njia ya mtandao hupunguza garama kubwa ya uendeshaji kibiashara kutokana na biashara za mitandao kuto hitaji eneo maalum la kufanyia biashara na kugarimu fedha kidogo na kuwafikia watu wengi zaidi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ukanda wa Afrika Mashariki, kutoka kampuni ya uuzaji
bidhaa kwanjia ya mtanda ya JUMIA – MARKET Bwana Justine
Christianson ameiambia East Africa Radio katika mahojiano maalum
kuusiana na biashara kwanjia ya mtandao, na kusema kuwa kunaurahisi
mkubwa kuendesha biashara mitandaoni.
“Huduma
za mtandao zinamrahisishia mteja kununua na kupata bidhaa kwa wakati
pamoja na kuepuka kutumia gharama za ziada kama usafiri kutokana na
wateja kupelekewa bidhaa majumbani mwao” amesema
Christians,
amesema katika nchi za Africa Mashariki Tanzania imeonekana kukuwa
kwa shuguli za kimtandao huku nchi ya Kenya ikiongoza kwakufanya
manunuzi mitandaoni ambapo aliwashauri vijana kutumia muda wao kubuni
njia za kujipatia kipato bila kugarimu fedha mitandaoni.
Meneja
Mkuu wa JUMIA MARKET nchini Tanzania Bwana Laurite Elmshauser amesema
ili kuhakikisha watanzania wengi wanatumia mitandao kununua bidhaa,
kampuni yao JUMIA imefanya punguzo la bei za bidhaa zake kwa asilimi
80 katika wiki yake ya maadhimisho ya Black Friday.
Meneja
Masoko wa JUMIA MARKET Bi. Herrieth ngolwa amesema kampeni hiyo
ijulikanayo kama Black Friday itakuwa ya siku 5 kuanzia Tarehe 21 Nov
hadi 25 Nov ili kuwawezesha watanzania kununua bidhaa za msimu wa
krismas kwa punguzo la pei kwa kutembelea mtandao wa JUMIA.
EmoticonEmoticon