Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally ametangaza siku kuu
ya kuzaliwa Mtume Muhamad ya Maulid maarufu kwa jina la Maulid Day,
kitaifa itasomwa siku usiku wa tarehe 11 mwezi wa 12 mwaka 2016
katika Mkoa wa Singida Wilaya ya Iramba.
Akiongea
na vyombo vya habari jijini Dar es salaam, Mufti Mkuu Sheikh Abubakar
Zubeir amesema Maulid ya mwaka huu yataadhimishwa kwa namna tofauti
ambapo waumini wa kiislamu kote nchini watatakiwa kuchangia damu na
kufanya zoezi la usafi katika maeneo yao mara tu baada ya ibada.
“Kipenzi
chetu Bwana Mtume Muhammad amesema “Uislamu ni Usafi basi
jisafisheni kwani hakika hataingia peponi isipokuwa Msafi, mwamisingi
hii mimi mwenyewe nitaongoza usafi kufurahia kuendana na kuiga na
kutekeleza mafundisho yake” amesema.
Aidha,
amewataka viongozi wa Baraza kusimamia na kuhimiza amani ya nchi yetu
na kutokuwa tayari kuwavumilia wale wote ambao wanataka kuharibu
amani na utulivu katika nchi yetu.
“Kauli
mbiu ya Maulid ya mwaka huu ni Muislamu jitambue badilika amani na
usalama ndio maisha yetu” hivyo nijukumu la kila muumini wa dini ya
kiislamu na waumini wa madheebu mengine kutunza amani. Amesema.
EmoticonEmoticon