Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo amemuapisha Kamishna wa
Polisi Diwani Athuman Msuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.
Hafla ya kuapishwa
kwa Kamishna Diwani Athuman Msuya imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed
Chande Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George
Mcheche Masaju, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu na Makamishna wa
Polisi.
Baada ya kuapishwa
kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya
amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Katibu wa
Sekretarieti ya Maadili, Idara ya Viongozi wa Siasa Bw. Waziri Yahaya Kipacha.
Kamishna wa Polisi
Diwani Athuman Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Amantius Msole
ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
EmoticonEmoticon