Muswada wa Sheria ya huduma ya msaada wa kisheria kujadiliwa


Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wadau wa masuala ya sheria na wananchi kwa ujumla kutoa maoni yao juu ya muswada wa sheria ya kusimamia na kuratibu utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria na kutambua wasaidizi wa kisheria, muswada ambao umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Dkt. Harrison Mwakyembe amesema muswada huo unalenga kusaidia zaidi wananchi wasiojua sheria, na wasio na uwezo wa kuwalipa wanasheria jambo ambalo litatimiza azma ya serikali ya watu wote kuwa sawa mbele ya sheria na kupata haki bila ubaguzi.

Dkt. Mwakyembe amesema ni vyema wasaidizi zaidi ya 80 ambao bado awajapewa mafunzo na kusajiliwa na wizara yake kufuata taratibu zilizowekwa na wizara yake kwani serikali bado inatambua msaada wao katika kuhakikisha kuwa wananchi wanaelimishwa kuhusu haki zao.

Naye Mratibu wa Sekretarieti ya msaada wa kisheria kutoka wizara ya Katiba na Sheria Bw. Daniel Lema amesema mara baada ya sheria hiyo kuanza kazi wananchi wataweza kupata wasaidizi wa kisheria katika maeneo yao kwani wizara hiyo itakuwa na uratibu mzuri wa kufanya kazi na mashirika ya sheria na wasaidia wa sheria.


EmoticonEmoticon