Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameonyesha kufurahishwa na hatua zinazochukuliwa na baadhi ya nchi za Afrika katika kulinda na kutetea haki za binadamu hasa haki za wanawake na kusema kuwa bado kuna umuhimu mkubwa kwa nchi ambazo zinazosuasua kutekeleza mikataba hiyo kufanya hivyo ili kuhakikisha wanawake na watoto wanapata haki sawa katika jami.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amesema kuwa, Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuwaajiri na kuwaingiza wanawake katika ngazi za maamuzi na kwa sasa mpango kabambe unafanyiwa kazi ili kuhakikisha sekta binafsi ambayo bado inaidadi ndogo ya wanawake kwenye ngazi za maamuzi kufanya hivyo.
Aidha amesema kuwa, tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini zinaonyesha kuwa wanawake wengi walioingizwa kwenye bodi mbalimbali tayari bodi hizo zimeongeza ufanisi wa kazi maradufu.
Kwa upande wake, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu Justice Sylvain Ore amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwani unalenga kujadili na kuweka mikakati inayolenga kuhakikisha nchi za Afrika zinazingatia na kulinda haki za bindamu hasa haki za wanawake kwa kiwango kikubwa.
Mkutano huo wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu ambao unafanyika Jijini Arusha umehudhuriwa na wajumbe kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakiwemo wajumbe kutoka Umoja wa Afrika AU na lengo la mkutano huo ni kutajadili masuala ya demokrasia na haki za binadamu katika nchi za Afrika.
EmoticonEmoticon