Wabunge wanaomiliki Mabasi ya Abiria waofiwa kuhujumu Muswada wa sheria za usafirishaji


Chama Cha kutetea  Abiria Nchini  Tanzania CHAKUA  kimemuomba Raisi Dr.John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,kuzuia wabunge wanaomiliki mabasi ya kusafirisha abiria kutoshiriki katika kujadili Muswada wa sheria za usafirishaji  kwa madai kuwa wanamaslahi yao binafsi hivyo watashiriki kukwamisha muswada huo.
Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti  Taifa wa CHAKUA, Bw.Hassani  Mchanjama,wakati akizungumza na wanahabari,ambapo pamoja na mambo mengine amesema kuwa wamiliki wa Mabasi ya kusafirisha abiria wakiwemo wabunge, wamekuwa wakipitish sheria mbovu  kwa lengo la kujinufaisha wenyewe bila ya kujali haki za abiria.
"Kila mara Sumatra wanapopeleka muswada kuusu marekebisho ya sheria za usafirishaji Wabunge wenye mabasi wanaukwamisha, wakati kunasheria mbivu mbovu za sekta ya usafirishaji hawana huruma kabisa na wananchi wanavyoteseka zaidi wanaangalia maslahi yao" amesema
Ameendelea kufafanua kuwa baadhi ya wakatishaji tiketi wanapandisha bei ya nauli kinyume cha kiwango ambacho kimewekwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya usafiri vya majini na nchi kavu(SUMATRA),ambapo ametolea mfano nauli za maeneo mengine hutozwa shilingi 35000/= badala ya shilingi 25000/= ambayo imepangwa na Sumatra.
Aidha ameendelea kufafanua kua CHAKUA  imeanzisha programu ya kuyafikisha mahakamani Mabasi yote yanayopata ajali na kusababisha madhara kwa  abiria,ili kusaidia abiria kulipwa fidia kwa urahisi na kwa muda mfupi.


EmoticonEmoticon