Asilimia 50 ya wananchi waliohojiwa katika
utafiti wa kubainisha ubora wa elimu katika shule za serikali tangu kuanzishwa
kwa mpango wa elimu bila malipo ya adda wamekiri elimu kuboreshwa licha ya kuwa
asilimia 60 ya wananchi kutamani kuwasomesha watoto wao katika shule binafsi.
Utafiti huo pia umebainisha kuwa asilimia
34 ya wananchi wamelalamikia ukosefu wa waalimu, asilimia 30 wamelalamikia ukosefu
wa madawati na asilimia 13 wakilalamikia ukosefu wa madarasa, wengine wakilalamikia ufundishaji na
ukosefu wa chakula kwa wanafunzi.
Mkurugezni mtendaji wa TWAWEZA Aidan
Eyakuze amesema idadi hiyo ni ya wananchi kati ya 1,806 waliohojiwa Tanzania
bara ambapo amesema asilimia 35 wamesema ubora wa elimu umemebaki palepale na
wengine asilimia 15 wamesema ubora umeshuka kabisa.
Adha Tafiti hiyo pia imebaini kua asilimia
85 ya wazazi hawajiusishi na masuala ya masomo ya watoto wao, huku asilimia 83
imekuwa ni changamoto za miundombinu na matokeo mabaya ya wanafunzi na utovu wa
nidhamu kwa wanafunzi
Utafiti huo umefanyika kati ya Agosti 7 na
14 mwaka huu hata hivyo baadhi ya wasomi walioshiriki uwasilishwaji wa ripoti
hiyo kutoka chuo kikuu cha elimu wamesema matokeo hayo ayaendani na uhalisia wa
hali ya elimu nchini na kwamba elimu aiwezi kuwanaubora kwa kipindi cha mwaka
mmoja pekee.
EmoticonEmoticon