Wizara ya mambo ya ndani nchini
Tanzania imetoa ufafanuzi juu ya tuhuma kadhaa za uonevu na
upendeleo, kuhusiana na zoezi linaloendelea hivi sasa la kuondoa
wahamiaji haramu katika maeneo mbali mbali hapa nchini
Hii leo Blog hii ilishuhudia raia
wa nchi mbalimbali miongoni mwao walikuwepo wamalawi zaidi ya 1500,
wa Nigeria na nchi zingine wakijiandikisha katika ofisi za uhamiaji
jijini Dar es salaam ili waweze kutambulika kisheria
Akiongea na thecampasvision
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi bwana Isaac Nantanga
amesema zoezi hilo ni endelevu na kuwa sio la kibaguzi na rushwa kama
ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakilalamika
Zoezi la wahamiaji harammu
litakuwa endelevu hasa jijini Dar es salaam, huku maeneo ya pembezoni
mwa nchi zoezi maalum litaendelea kwani maeneo hayo yanaongoza kwa
kuwa na wahamiaji haramu.
Hapo jana baadhi ya wananchi
kutoka kigoma na baadhi ya wabunge wao walikutana katika eneo la
Tegeta kujadili suala hilo ambapo walidai kuwa zoezi hilo linafanywa
kibaguzi na rushwa kitu ambacho wizara ya mambo ya ndani ya nchi
imekikanusha.
EmoticonEmoticon