MAONYESHO YA BIDHAA ZA WACHINA YA FUNGULIWA


 Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda hii leo amefungua maonyesho ya bidhaa za wachina kwa nchi za Afrika yanayofanyika jijini Dar Es Salaam kwa siku tatu yakiwa na lengo la kubadilishana ujuzi wa kutengeneza bidhaa mbali mbali na kuwapa uwezo wazalishaji katika nchi za afrika.

Akiongea katika ufunguzi huo, Mhe. Pinda amewataka wafanyabiashara hasa wa Tanzania kutumia vizuri fursa hii ili kuendeleza uchumi na kupanua wigo wa biashara ndani na nje ya Nchi.


Ufunguzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali nchini akiwemo Waziri wa viwanda na biashara Mhe. Abdallah Kigoda, pamoja na Kaimu mkurugenzi wa Wizara ya biashra bwana Zhang Xialing ambapo viongozi hao wamesisitiza kuwepo kwa mbinu mpya zitakazoweza kunufaisha nchi za Afrika kiuchumi.

MFUMUKO WA BEI UMESHUKA KWA MWEZI JUNE,2013 OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAELEZA

Kushuka kwa bei za bidhaa za vyakula hapa nchini imechangia kushuka kwa mfumuko wa bei za bidhaa hizo kwa mwezi Julai 2013 hali iliyopelekea hali ya uchumi kwenda vizuri hivi sasa.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu, Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii bwana Ephraim Mwesigabo, amesema kwa sasa bei ya bidhaa za chakula imeshuka lakini kwa bidhaa zisizo za chakula bei imebaki kuwa juu.

Aidha bwana Ephraim ameongeza kuwa tathmini ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi Agost 2013 ikilinganishwa na mwaka 2010 dhidi ya fedha za nchi jirani za Afrika Mashariki umebaki kuwa vile vile na kuwa bei ya mfumuko wa bei kwa nchi hizi uko sawa.

Ephraim amewataka watunga sera pamoja na watanzania wote kujali kuwa na Elimu ya viwango vya fedha pamoja na mfumuko wa bei ambayo inatolewa mara kwa mara na ofisi hiyo.


EmoticonEmoticon