WANANCHI WATAKIWA KUTOA MAONI MPANGO WA OGP


MWALIKO KWA WADAU KUCHANGIA MAONI KATIKA ZOEZI LA SERIKALI
KUJITATHMINI (SELF ASSESSMENT) KATIKA UTEKELEZAJI WA
MPANGO WA UENDESHAJI SHUGHULI ZA SERIKALI KWA
UWAZI (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP)


Serikali kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia (Civil Society Organizations) inatakiwa kufanya zoezi la tathmini (Self Assessment) ili kujua ni kwa kiwango gani ahadi zilizoainishwa katika mpango wa OGP zimetekelezwa.

Serikali imeanza kutekeleza ahadi (commitments) zilizoainishwa katika Mpango Kazi wake katika sekta tatu za kipaumbele za huduma za Afya, Elimu na Maji. Serikali imetekeleza ahadi zilizoainishwa katika Mpango Kazi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai, 2012 hadi Julai, 2013. Kwa mujibu wa matakwa ya Mpango wa OGP,

Kwa hiyo wadau wote na wananchi kwa ujumla wanakaribishwa kuchangia maoni ya jinsi mipango kazi ya OGP ilivyotekelezwa kwa kujaza fomu iliyopo kwenye tovuti www.ega.go.tz/ogp.

Mwaka 2011, Serikali ya Tanzania ilijiunga na Mpango wa Kimataifa wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership - OGP). Uamuzi huu wa kujiunga na Mpango wa OGP unalenga kuongeza juhudi za Serikali katika kuweka uwazi zaidi katika uendeshaji wa shughuli zake; 

kushirikisha wananchi katika upangaji na utekelezaji wa shughuli za Serikali; kuimarisha uwajibikaji katika utendaji wa Serikali; kuimarisha juhudi za kuzuia na kupambana na rushwa na kuweka umuhimu wa matumizi ya teknolojia na ubunifu.

Maoni hayo ni muhimu katika kufanikisha zoezi la Serikali la kujitathmini na pia katika kuboresha maandalizi ya Mpango Kazi utakaotekelezwa katika kipindi kinachofuata cha miaka miwili kuanzia 2014 – 2016. Maoni yawe yamewasilishwa kabla ya tarehe 18 Septemba, 2013.



EmoticonEmoticon