KESI DHIDI YA PINDA NA KAULI YA PIGA TU, WALALAMIKAJI WAAMBIWA HAWANA HAKI YA KUSHITAKI



Mahakama kuu ya Tanzania hii leo imetoa siku 14 hadi Octoba 18 mwaka huu kwa kituo cha sheria na haki za binadamau LHRC na chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS 



kujibu hoja za serikali waliofungua didhi ya Waziri mkuu Mizengo Pinda.

Katika shauri hilo, kituo cha sheria na haki za binadamu na chama cha wanasheria wa Tanganyika kwa pamoja wanaitaka mahakama kuu itamke kuwa waziri mkuu alivunja katiba na kumtaka Waziri mkuu Mizengo Pinda afute kauli aliyoitoa bungeni ya kuvitaka vyombo vya dola vipige wananchi

Akizingumza na Blog hii mara baada ya shauri hilo katika mahakama kuu, mwanasheria wa upande wa mashtaka Bw. Fulgence Massawe amesema wanaenda kujipanga kujibu hoja hizo na kwamba wana imani mahakama itatenda haki juu ya madai yao

“Pingamizi huwa kikawaida na sisi tunajipanga kujibu hoja tano juu ya madai yetu ifikapo Sept. 30 kama ambavyo mahakama imetutaka kufanya” Alisema Fulgence

Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji kiongozi Fakihi Jundu limeutaka upande huo wa mashataka kujibu hoja tano zilizo tolea na serikali, mojawapo ikiwa ni ile inayodai kuwa waliofungua kesi hawana haki kisheria kufungua kesi hiyo

Katika bunge la Bajeti kwa mwaka wa fedha 2013/2014 katika kipindi cha maswali na majibu waziri mkuu akijibu swali bungeni akisema polisi wa pige tu kwani hawana njia nyinge na mtu atakefanya fujo atapigwa tu, muwapige tuu. Kauli ambayo imepelekea kiongozi huyo kufunguliwa mashitaka ya kuvunja katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.


EmoticonEmoticon