Baadhi
ya wilaya hapa nchini bado zinakabiliwa na ukosefu mkubwa wa
mahitaji ya huduma za afya kama vile ukosefu wa madawa, madaktari
pamoja na vifaa vya matibabu kituambacho kinarudisha nyuma juhudi za
kupambana na vifo vya mama na mtoto hapa nchini
Hayo
yamebainishwa leo katika mkutano uliokuwa unajadili maendeleo ya
mradi wa kuboresha afya,
Ya watoto walio chini ya miaka 5 na akina
mama wajawazito unaotekelezwa katika wilaya za Same, Kilindi na
Arusha vijijini chini ya shirika la World Vision.
Mganga
mkuu wa wilaya ya Kilindi Dkt Abbas Mungia, amesema wilaya yake
inaukosefu mkubwa wa wakunga, madawa na wakati mwingine yale yanayo
patikana yapo chini ya viwango vya wizara ya afya ambavyo vinataka
viwepo katika maeneo ya Wilaya, kata na vitongoji
Aidha
amratibu wa masuala ya Afya katika shirika la World Vision bi. Agnes
Victor amesema shirika hilo linahakikisha vifo vyao mama na mtoto
vinapungua kufikia kwa asilimia 93% ifikapo mwaka 2015.
Wizara
ya Afya hapa nchini pamoja na mashirika mbalimbali ya Afya yanafanya
juhudi ilikuweza kupunguza vifo vya mama na mtoto ambavyo vinatokea
kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kina mama kutohudhuria
kliniki, kuto jifungua katika vituo vya afya, huduma mbovu za afya
pamoja na upungufu wa wauguzi.
EmoticonEmoticon