CHAMA CHA WALIMU CHAZIDI KULIA NA SERIKALI JUU YA MADAI YAO

Mwenyekiti wa chama cha waalimu nchini bwana Gratius Mukoba ameitaka serikali kuwalipa walimu madai yao yanayofikia kiasi cha shilingi Billioni 40 hivi sasa ili kuwepo na utekelezaji mzuri wa mpango wa maendeleo makubwa sasa katika sekta ya elimu nchini.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, bwana Mukoba amesema wanategemea madai yao kushugulikiwa mapema kabla ya kikao hicho na kuongeza kuwa matarajio ya waalimu wote nchini ni kuona madai hayo yanapatiwa ufumbuzi.


Tunataka ufumbuzi wa madai yetu kwani ni muda sasa tunamgongano na serikali ikafikia kufikishwa mahakamani kiasi kwamba madai ya walimu yakaonekana hayana maana, na mahakama kuitaka serikali kukaa na sisi meza moja kujadili madai yetu. Alisema mukoba
Mukoba aliongeza kuwa, hivi sasa serikali inatekeleza matokeo makubwa sasa bila kuyashugulikia madai ya walimu wakati ndio watekelezaji wakwanza wa hilo suala ..bila Big salary now hakuna Big result now bali kutakuwa na Big result now. amesema Mukoba
Madai ya walimu yakulipwa mshahara kwa kiwango cha asilimia 100, haikuwa jinsi watu walivyo tafsiri kwani kiwango hicho ilikuwa sawa na laki 4, ambacho ni sawa na posho ya mbunge kwasiku. Alisema Mukoba
Aidha, bwana mukoba ameeleza baadhi ya maoni ya waalimu katika rasimu ya katiba mpya kuwa ni kutaka kuundwa kwa tume ya kikatiba itakayoshugulikia madai ya watumishi wa Elimu ili kuondoa usumbufu uliopo sasa ambapo wanajikuta wakienda katika idara mbalimbali kudai madai yao.
"Kuwepo na tume ya kikatiba itakayo shugulikia madai ya wafanya kazi wa sector ya elimu, kwani hivi sasa mara uende tamisemi na maeneo mengi kisi kwamba inakuwa usumbufu kushugulikiwa madai ya wali kikamilifu"Amesema Mukoba
Kwa muda mrefu sasa walimu wamekuwa katika mgogoro na serikali wakiwa na madai mbalimbali hasa ongezeko la mishahara kufikia asilimia 100 lakini mpaka sasa serikali imewaongeza mshahara kwa asilimia 8 tofauti na asilimia 65 ambayo walikubaliana baada ya mgogoro wa muda mrefu.


EmoticonEmoticon