Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Alhamisi, Septemba 5, 2013, amekutana kwa faragha na Rais wa
Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri
na kuwaridhisha viongozi hao wawili wa nchi jirani.
Viongozi
hao wamekutana kwa saa moja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli
ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa Kampala,
Uganda.
Katika
mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea
kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo
kati ya nchi hizo mbili.
Viongozi
hao wawili wako nchini Uganda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa
Umoja wa Kimataifa wa Maziwa Makuu – “International
Conference on the Great Lakes Region (ICGLR)”
unaofanyika leo Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort.
Viongozi
wengine ambao wanahudhuria Mkutano huo ni pamoja na Rais Yoweri
Museveni wa Uganda ambaye ni Mwenyekiti wa ICGLR na mwenyeji wa
Mkutano huo, Rais Silva Kiir wa Sudan Kusini, Rais Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Mwenyekiti wa Kamisheni ya
Umoja wa Afrika (AU).
Rais
Kikwete na ujumbe wake amewasili Kampala asubuhi ya leo akitokea
mjini Dodoma ambako aliwasili jana jioni kwa ajili ya hafla ya
kuwaapisha Makatibu Wakuu watatu na Naibu Makatibu Wakuuu wawili
iliyofanyika Ikulu Ndogo, Dodoma.
Rais
Kikwete aliwasili Dodoma akitokea Mwanza ambako alihudhuria mazishi
ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Evangelistic
Assemblies of God Tanzania (EAGT)
Askofu Mkuu Dkt. Moses Samwel Kulola yaliyofanyika kwenye Kanisa la
Bugando Calvary Temple, mjini Mwanza.
Imetolewa
na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
05
Septemba, 2013
EmoticonEmoticon