WANAOSEMA TUME YA UCHAGUZI SIO HURU, NI WAONGO !

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania imesema ina uhuru wa kutosha kuendesha chaguzi mbali mbali ikiwamo kura ya maoni ya katiba mpya, tofauti na ambavyo wadau wengi wamekuwa wakidai kuwa tume hiyo sio huru.

Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam kufuatia kile alichodai kuwa ni mfululizo wa madai potofu kutoka kwa baadhi ya wanasiasa na  wadau wa demokrasia na uchaguzi, ambao wamekuwa wakimnukuu yeye eti akidai kuwa tume yake haipo huru.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Jaji Lubuva amesema hakuna kiongozi yoyote aliyewahi kuingilia utendaji wa tume hiyo na kwamba hivi sasa inafanya maandalizi kwa ajili ya kusimamia zoezi la kura ya maoni ya katiba mpya pamoja na kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya chaguzi zijazo.


EmoticonEmoticon