BEI ZA UMEME JUUU...... TANESCO YAZIDI KULEMEWA NA MADENI SASA YAFIKIA BILIONI 456.8 MIZIGO WABEBESHWA WANANCHI.

Mamlaka wa udhibiti wa nishati na maji EWURA hii leo jijini Dar es salaam wametangaza kupanda kwa bei za umeme ifikapo Januari 1. 2014 kutoka asilimia 67.87 kutoka asilimia 40.29 bei inayotumika hadi hivi sasa.


 Akitangaza ongezeko la bei hizo Mkurugenzi wa udhibiti uchumi wa EWURA Bwana Felix M.Mngamlagosi amesema wamepandisha bei hizo kutokana na Tanesco kuelemewa nakuwa shirika hilo lina hali mbaya kifedha.



"EWURA imebaini kwamba hali ya kifedha ya shirika la umeme sio nzuri kwani limeendelea kupata hasara ya shilingi Bilioni 47.3 katika mwaka 2010 mpaka kufikia Bilioni 223.4 mwishoni mwa mwaka 2012, hivyo kuinusuru shirika hilo tumekubaliana kuongeza bei za umeme"amesema Felix

Pamoja na mapungufu ya kiufanisi, garama za uzalishaji wa umeme ambao Tanesco inanunua kutoka kwa wazalishaji binafsi ndio imesababisha shirika hilo kushindwa kulipa madeni yake ya muda mfupi na muda mrefu.

"Madeni yaliyo limbikizwa katika shirika hili kwa mwaka huu 2013 yamefikia Billioni 456.8 hali ambayo inatishia uendelevu wa huduma za umeme hapa nchini" amesma Felix

Akielezea juu ya kanuni zilizo tumika na mamalaka hiyo kupandisha bei hizo bwana Felix amesema kuwa, EWURA wametumia kanuni ua ukokotoaji bei kama ilivyo pendekezwa na AFRMERCADOS wakati wa kukokotoa mahitaji ya mapato ya TANESCO kanuni hiyo imewezesha kukokotoa bei zinazo landana na garama halisi kwenye mfumo wa umeme na kuzigawa kwenye makundi ya watumiaji umeme, kadiri kila kundi linavyo sababisha gharama kwenye mfumo wa umeme kwa mujibu wa mahitaji ya sheria ya umme ya 2008 kifungu cha 23(2)(f).

Aidha EWURA imetaka TANESCO kuzalisha umeme kwa kutumia mitambo yenye gharama nafuu, kuhakikisha kuwa zabuni za miradi ya uzalishaji umeme zinatolewa kulingana na mahitaji kama ilivyo idhinishwa kwenye mpango wa umeme wa Taifa, Kuwasilisha ripoti kila baada ya miezi mitatu kuhusu viashiria vya takwimu za ubora na uhakika wa umeme.

Tarehe 11 Octoba 2013 shirika la umeme Tanzania TANESCO liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa mamlaka ua udhibiti wa huduma za Nishati na Mmaji EWURA. TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67. 87 kuanzia tarehe 1. Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 January 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 January 2015.

Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na m,abadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya Kitanzabnia.

Aidha TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyo zingantia ruzuku inayotolewa na serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO
 


EmoticonEmoticon