Takribani ekari laki nne za misitu huteketea kila mwaka nchini Tanzania, kutokana na vitendo mbali mbali vya uharibifu wa mazingira unaoendana na uchomaji moto misitu pamoja na ukataji miti hovyo. Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya misitu katika wizara ya maliasili na utalii, Nurdin Chamuya, amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya matumizi endelevu ya mazao ya misitu, kampeni inayoendeshwa na MAMA MISITU, mradi unaoboresha utawala wa misitu kwa manufaa ya wananchi. Kwa mujibu wa Chamuya, asilimia 55 tu ya ardhi yote ya Tanzania ndio imefunikwa na misitu na kwamba jumla ya fedha za Tanzania shilingi bilioni 6.8 zinapotea kila mwaka kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya misitu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon