RIPOTI YA TOKOMEZA UJANGILI YA THIBITISHA SERIKALI KUUSIKA NA VITENDO VYA MAUAJI, UBAKAJI, UDHALILISHAJI NA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

JK APEWA RUNGU KUAMUA,
PINDA NAYE MAJI YA SHINGO,
MAWAZIRI WA 4 MATUMBO JOTO BUNGE LATAKA WAVULIWE MADARAKA,WAMTAKA KAMANDA ALIYE SIMAMIA ZOEZI HILO..........


Kutoka Bungeni Dodoma




Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hii leo wameungana na kukemea matendo ya kikatili yaliyofanya kipindi cha zoezi la “TOKOMEZA UJANGILI ” na kumtaka Waziri mkuu Mhe. Mizengo Pinda kujiuzulu wadhifa wake kwa kushindwa kuwa simamia Mawaziri ambao zoezi hilo lilifanywa chini ya Wizara zao.


Mawaziri hao ni Mhe. Shamsi Vuai Nahodha ambaye ni Waziri wa Ulinzi, Mhe Emmanuel Nchimbi ambaye ni Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Hamis Kagasheki ambaye ni Waziri wa Maliasili na utalii na Mhe. Mathayo David Mathayo ambaye ni Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo

Ripoti iliyo somwa mbele ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Mhe. James Lembeli kamati hii ni maalum kwa ajili ya kusimamia serikali kwa upande wa wizara ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambayo imebaini ukatili mkubwa na udhalilishaji waliofanyiwa watanzania kipindi cha Zoezi la Tokomeza ujangili

Vitendo vya kikatili ambavyo walikuwa wakifanyiwa watu ni UBAKAJI, UKATILI, UDHALILISHAJI NA HATA MAUAJI YA WATU huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu, hivyo bunge limewataka viongozi wanao husika wajiuzulu kwakushindwa kuwajibika kwenye nafasi zao kiasi cha kupelekea vifo kutokea mikononi mwa vyombo vya dola ambayo inatafsiri ya (serikali) hivyo kumtaka Mhe. Mizengo Pinda naye ajiuzulu kwa kashfa hii



RAIS JK ATAKIWA KUINGILIA KATI NA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU


Wabunge mbalimbali walitaka mhe. Rais afanye maamuzi ya kuwavua madaraka viongozi hao ilikuonyesha kuchukizwa kwa vitendo hivyo nakuwa serikali haiusiki na mauaji dhidi ya raia wake


Nukuu ya Wabunge Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, Mhe. James Mbatia” na wengine wengi ambao walikuwa na kauli moja Wamesema kuwa “Mwanamke mmoja akibakwa wote wanaumia, mtanzania mmoja akiuwawa wote wanaumia... wengine walidai kuwa kwanini “Tanzania iwe na maeneo ya mateso kama Guantanamo Bay hivyo nilazima Rais awawajibishe.


Ni mara chache sana katika vipindi mbalimbali vya Bunge kwa wabunge wote kuungana na kutoa sauti zemnye hoja moja na kuaweka Upinzani pembeni, Hii leo wabunge wa Tanzania wametaka huruma na haki itendeke kwa watanzania walitendewa unyama huu


Hivyo kulingana na mikataba ya kimataifa Rasi atatakiwa kutenda haki kwani sheria za haki za binadamu zaweza iangukia serikali yake kwa kuruhusu mauaji ya raia.


Zoezi la tokomeza ujangili lilianzishwa kwa lengo la kutokomeza ujangili na mauji ya tembo kitu ambacho hakikufanikiwa na badala yake mauaji yakageuzwa kwa mifugo na Raia. Ripoti pia imebaini Mawaziri na Wabunge, Vyama vya siasa kuhusika katika kuharibu zoezi hilo.


Watanzania wengi wanasubiri maamuzi ya Rais Jakaya Kikwete juu ya mawaziri wake ambao wameruhusu mauaji kutokea kipindi cha zoezi hilo huku wizi na mauaji ya wanyama bori yakiwa palepale.




HITIMISHO, Ni vyema yote yaliotolewa ushauri yafanyiwe kazi, sheria ichukuwe mkondo wake, viongozi waliowajibika wajiuzulu ili serikali ijitoe katika mkono huu wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kujiondoa katika kashfa hii ya mauaji kwani Idara ya Usalama, Ulinzi nayo imehusika katika ukatili huu Mawaziri wamo serikali ni vyema ikajisafisha kuepuka lawama kubwa kwa wananchi wake ambao wamezidi kulia mamchozi baada ya ripoti hii kutolewa hadharani


EmoticonEmoticon