SERIKALI YASEMA ITAHAKIKISHA FEDHA ZA MAENDELEO ZINAWAFIKIA WALENGWA

Serikali ya Tanzania inajipanga kuchukua hatua endelevu katika kuhakikisha fedha kwa ajili ya maendeleo zinazotengwa kwa kila sekta zinafikia walengwa kwa wakati.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda ameyasema hayo jana Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la mbunge Mhe. Nkumba aliyetaka kufahamu ni lini serikali itaweza kufanikisha kupeleka fedha za maendeleo kwa wakati  hasa za serikali kuu.

Mhe. Pinda amesema kuwa tatizo hujitokeza zaidi katika robo ya kwanza ya mwaka ambapo makusanyo yanakuwa hafifu, hata hivyo serikali inajipanga kutatua tatizo hilo.


EmoticonEmoticon