ONDOA VIKWAZO FUNGUA MILANGO YA KUJENGA JAMII JUMUISHI KWA WOTE


Watu wenye ulemavu wametakiwa kutokuwa wanyonge na badala yake wajitokeze na kujishugulisha na shuguli mbali mbali katika jamii

Hayo yamesemwa na Mratibu wa kitengo cha walemavu kutoka hosptali ya CCBRT bwana Fredrick Msigana wakati akiongea na Blog hii mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

Bwana Fredrick amesema walemavu wamekuwa wanyonge kila mara hivyo wanakosa fursa zingine ambazo wangeweza kujitokeza kuzifanyia kazi na kusema kuwa siku ya walemavu duniani itakuwa fursa kubwa kwao

“Walemavu wajitokeze walete kazi zao kwenye maadhimisho ya siku ya walemavu duniani tarehe 03. Dec hapa kuna wananchi wengi watahudhuria hivyo kazi zao zinaonekana” Alisema Fredrick

Aidha Fredrick alisema, kauli mbiu katika siku hiyo ni Ondoa vikwazo fungua milango kujenga jamii jumuishi kwa wote.

Tanzania kama nchi zingine duniani hapo kesho itaadhimisha siku ya walemavu duniani, ambayo nikila tarehe 3 Dec.

Zaidi ya watanzania Milioni 3,456,900 ni walemavu wa akili, viungo, kuona,kusikia na aina nyingine za ulemavu idadi inayoongezeka siku hadi siki

Kundi hili linakabiliwa na matatizo mengi katika jamii ikiwa kama unyanyapaa, miundo mbinu isio rafiki kwao, kutopewa elimu na ajira kama watu wengine hivyo jamii na serikali inapaswa kuondoa vikwazo ili tuwe na jamii yenye usawa kwa wote.




EmoticonEmoticon