HAPA KAZI TUU.... JOHN POMBE MAGUFULI AANZA NA WIZARA YA FEDHA
Rais
wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli hii leo
amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Wizara ya fedha na
kukuta baadhi ya watendaji katika Wizara hiyo wakiwa hapo ofisini
Ikiwa bado ni muda wakazi.
Katika
hali isiyoyakawaida, Rais Magufuli pia alitembea kwa miguu akitokea
Ikulu kwenda ofisini hapo akiambatana na walinzi wake ambapo alikuta
maofisa hao wakiwa awapo kazini.
Hivyo kumtaka Mhe Rais JP kuhakikisha kuwa anafanya ziara za mara kwa mara ili aweze kuwawajibisha wafanyakazi wazembe serikalini.
JANET MBENE WASHUKURU WANANCHI WA JIMBO LA SONGWE KWA KUMPA KURA ZA KISHINDO
MBUNGE mteule katika Jimbo la Ileje mkoani Songwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mbene (CCM) amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumpa kura za kishindo, madiwani na Dkt. Jonh
Magufuli anayewania urais.
Akizungumza na wakazi wa Ileje, Mbene alisema ushindi wa kura 27,583 aliopewa na wana Ileje dhidi ya Emmanuel Mbuba wa NCCR Mageuzi aliyepata kura 14,578
atahakikisha anawapa wananchi hao kupitia ushirikiano, usimamizi na utatuzi wa changamoto mbalimbali
zinazowakalibi.
“Awali ya yote niwashukuru wana Ileje kwa kuonesha imani kubwa kwangu, madiwani na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Jonh Magufuli. Wana Ileje wametupa kura za kishindo nami ninawahaidi sitawaangusha katika utekelezaji wa ahadi nilizozitoa kwenu wakati wa kampeni,”
alisema Mbene.
CD ZISIZO NA CHATA YA TRA KUPIGWA STOP JULY MOSI
Baraza la sanaa Tanzania kwa kushirikiana na Baraza la hatimiliki nchini zimejipanga kuzuia mauzo ya CD za wasanii wa bongo ambazo hazina chata ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), ili kuongeza kipato cha wasanii na Taifa kwa ujumla.
Wakiongea na Blog hii leo Dar es salaam, Kaimu katibu mtendaji wa BASATA bwana Godfrey Lebejo na Mtaalamu wa Tehama kutoka COSOTA wamesema zoezi hilo litaanza rasmi July 1 mwaka huu.
Kwa muda sasa wasanii wa bongo wamekuwa wakilalamika kuibiwa kazi zao, hivyo mamlaka hizi zimeamua kutumia mbinu mpya ya kudhibiti kazi hizo kwa lengo la kuinua maslahi ya wasanii.
TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR (ZEC) IMEFUTA MATOKEO YA UCHAGUZI
Mwenyekiti
wa tume ya uchaguzi zanzibar salim jecha salim ametangaza kufutilia
mbali matokeo ya uchaguzi visiwani humo kwa madai kuwa kumekuwepo kwa
kura nyingi kuliko idadi iliyopo kwenye daftari la wapiga kura.
Akitangaza
suala hilo mwenyekiti wa zec amesema kumetokea kuwepo kwa dosari
nyingi kwenye upigaji kura jambo ambalo amelitaja kuwa sio wa haki.
"Kumegundulika
kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa
baadhi ya vituo vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura
wa kituo husika." amesema salim jecha
Amesema
hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba "baadhi ya
wapiga kura hawakwenda kuchukuwa vitambulisho vyao vya kupigia kura".
WATU WANNE WAKAMATWA KWA KUNUNUA KADI YA MPIGA KURA MOROGORO
Ikiwa imebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu katika hali isiyo ya kawaida watu wanne wasiofahamika itikadi zao za kisiasa wamekamatwa na wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) kwa madai ya kupita katika kata za manispaa ya morogoro na kudai shahada za wapiga kura kwa nguvu na kuanza kuorodhesha majina ya wananchi na namba zao za simu
kwa upande wananchi mashuhududa waliokumbana na watu hao katika harakati za kuwaandikisha wapiga kura majina wameeleza jinsi watu hao walivyokuwa wakifanya zoezi hilo kwa kudai kwa lazima shahada za kupigia kura ambapo baadhi ya watu walikubali na wengine wafikisha jambo hilo kwa afisa mtendaji wakata na wananchi waliamua kuungana na kuwakamata na kisha kuwapeleka katika kituo cha polisi cha mji wa morogoro.
MHE. DEO FILIKUNJOMBE AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NDEGE
Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la ludewa kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi ccm mhe. deo filikunjombe na wengine watatu wamefariki dunia katika ajali ya chopa iliyotokea eneo la hifadhi ya selous
Akidhibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamishna wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi poul chagonja amesema ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria wanne wakitokea dar es salaam kuelekea njombe na waliotambuliwa mpaka sasa ni rubani wa ndege hiyo capten willium silaa na deo filikunjombe
Kamishna
chagonja amesema jeshio la polisi limaendelea na uchunguzi wa ajali
ya ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y DKK unaendelea na kuwa abiria
wengine wawili bado hawajatambuliwa kwa majina yao.
sauti
ya kamishna chagonja akielezea zaidi
BUNGE LAVURUGIKA NA KUAHIRISHWA , KAULI YA WAZIRI MKUU MHE. PINDA YASUBIRIWA KWA HAMU
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo asubuhi amelazimika
kusitisha shughuli za bunge baada ya wabunge kutaka serikali
kuahirisha mchakato wa kura ya maoni pamoja na kutoa taarifa ya
uandikishwaji wa wapigakura kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa
BVR.
Wakichangia
hoja bungeni Mbunge wa Kisarawe Mh. Suleiman Jaffo na Mbunge wa
Ubungo Mh. John mnyika wametaka suala hilo lijadiliwe kama dharura na
kutolewa majibu na serikali kuhusu hatama ya mchakato huo.
Taharuki
ilizuka baada ya Spika wa Bunge hilo Mhe. Makinda kutaka kuzitupilia
mbali hoja hizo. Wabunge walianza kupiga kelele kutaka majibu ya
serikali papo hapo na ndipo Spika wa bunge alilazimika kuhairisha
kikao hicho mpaka jioni ambapo leo ni kikao cha mwisho cha bunge
hilo.
“ Mnyika
“ Nimesimama kupata Idhini kwa mujibu wa kanuni kuomba shuguli za
mbunge zisitishwe na badala yake tujadili zoezi la uandikishwaji
kwani mpaka sasa zoezi halijakamalika hata kwa mkoa mmoja, hivyo
Waziri mkuu kwakuwa yupo hapa Bungeni atupe majibu nini kinaendelea”
Amesema Mnyika
Spika
“Hoja hii na ile ya kwanza zinafanana, majibu mtajibiwa baadae
katika kikao cha jioni” Alisema spika. Aidha wabunge wa Upinzani
walionesha nia ya kutaka kujua hivyo kupiga kelele kwakusema “Tuna
taka Majibu” hali iliyopelekea spika wa bunge kuahirisha Bunge hadi
jioni.
MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa.
Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa afisa mnadhimu mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gemini Mushi. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola anakwenda kuwa Kaimu Kamishna wa Intelijensia makao makuu.
Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maria Nzuki amehamishwa makao makuu kuwa mkuu wa polisi jamii na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha ufundi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya.
Wengine ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Godfrey Kamwela amehamishiwa Polisi Makao Makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fulgence Ngonjani.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa mkuu wa utawala na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Mohamed.
Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa.
Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa afisa mnadhimu mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gemini Mushi. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola anakwenda kuwa Kaimu Kamishna wa Intelijensia makao makuu.
Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maria Nzuki amehamishwa makao makuu kuwa mkuu wa polisi jamii na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha ufundi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya.
Wengine ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Godfrey Kamwela amehamishiwa Polisi Makao Makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fulgence Ngonjani.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa mkuu wa utawala na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Mohamed.
JIHADHARI NA MATAPELI AJIRA ZA WALIMU WAPYA 2016, SOMA HAPA
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA
KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA
SHULE
ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU
MWAKA
2015/16.
JIHADHARI NA MATAPELI
Kumekuwepo
na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya kwa mwaka
2015/16 (TANGAZO
No. T.022/15TMS 2015)
linalodaiwa kuwa limetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
na kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii. Taarifa zilizotolewa katika
tangazo hilo siyo za kweli na Wizara haihusiki nazo.
Aidha,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda kuufahamisha umma kuwa
ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti, Stashahada, na Shahada hufanywa na
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira
kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.
Kutokana
na mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa sahihi kuhusu
ajira mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha zitatangazwa na Mamlaka
inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI mara
watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.
Imetolewa
na:
Katibu
Mkuu,
WIZARA
YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
23
Machi, 2015
TCRA YATOA MAAGIZO KWA MAKAMPUNI YA SIMU JUU YA TOZO ZA VIFURUSHI VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI
KUHUSU TOZO KWENYE
SEKTA YA TEHAMA
Katika
wiki ya pili ya Februari 2015, baadhi ya watoa huduma za mawasiliano
ya simu za mkononi walianzisha vifurushi vya mawasiliano na bei na
kusabababisha malalamiko kutoka kwa watumiaji na umma kwa ujumla.
TCRA, kwa kuzingatia upeo wa shughuli zake, imechambua hali hiyo na
inapenda kutoa maelezo na maagizo ambayo yatawezesha kuondoa
sintofahamu iliyopo na kujenga mustakabali kwa siku zijazo.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003,
miongoni mwa kazi za TCRA ni kufuatilia utoaji wa huduma katika
sekta inazozisimamia kwa kuzingatia kiwango cha upatikanaji wa huduma
hizo, ubora na viwango vya huduma, bei ya huduma na kuhimiza
ushindani na ufanisi wa kiuchumi. Katika kutelekeza majukumu yake,
TCRA inawajibika kupitia na kuchambua, mara kwa mara, utoaji wa
huduma katika sekta na kuchukua hatua dhidi ya chochote kinachotokea
kwenye soko, kiwe chanya au hasi.
Subscribe to:
Posts (Atom)