JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA
KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA
SHULE
ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU
MWAKA
2015/16.
JIHADHARI NA MATAPELI
Kumekuwepo
na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya kwa mwaka
2015/16 (TANGAZO
No. T.022/15TMS 2015)
linalodaiwa kuwa limetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
na kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii. Taarifa zilizotolewa katika
tangazo hilo siyo za kweli na Wizara haihusiki nazo.
Aidha,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda kuufahamisha umma kuwa
ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti, Stashahada, na Shahada hufanywa na
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira
kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.
Kutokana
na mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa sahihi kuhusu
ajira mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha zitatangazwa na Mamlaka
inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI mara
watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.
Imetolewa
na:
Katibu
Mkuu,
WIZARA
YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
23
Machi, 2015
EmoticonEmoticon