TCRA YATOA MAAGIZO KWA MAKAMPUNI YA SIMU JUU YA TOZO ZA VIFURUSHI VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI


KUHUSU TOZO KWENYE SEKTA YA TEHAMA

Katika wiki ya pili ya Februari 2015, baadhi ya watoa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi walianzisha vifurushi vya mawasiliano na bei na kusabababisha malalamiko kutoka kwa watumiaji na umma kwa ujumla. TCRA, kwa kuzingatia upeo wa shughuli zake, imechambua hali hiyo na inapenda kutoa maelezo na maagizo ambayo yatawezesha kuondoa sintofahamu iliyopo na kujenga mustakabali kwa siku zijazo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, miongoni mwa kazi za TCRA ni kufuatilia utoaji wa huduma katika sekta inazozisimamia kwa kuzingatia kiwango cha upatikanaji wa huduma hizo, ubora na viwango vya huduma, bei ya huduma na kuhimiza ushindani na ufanisi wa kiuchumi. Katika kutelekeza majukumu yake, TCRA inawajibika kupitia na kuchambua, mara kwa mara, utoaji wa huduma katika sekta na kuchukua hatua dhidi ya chochote kinachotokea kwenye soko, kiwe chanya au hasi.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaongozwa na Sera za Kisekta, Sheria ya Mamlaka ya Mawasilioano Tanzania ya 2003, Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010, na Kanuni zake za mwaka 2011 zilizotungwa kwa kuzingatia matakwa ya EPOCA. Kifungu 6(1) cha Sheria ya TCRA kinaitaka Mamlala kufuatilia utoaji wa huduma unaofanywa na sekta inazozisimamia ikiwa ni pamoja na upatikanaji, ubora na viwango vya huduma, gharama za huduma hizo na kufanikisha ufumbuzi na utatuaji wa malalamiko na migogoro. Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kuhusu tozo mpya zilizotangazwa na makampuni ya simu za mkononi.
  1. UKUAJI WA SEKTA YA TEHAMA
Kumekukuwepo na kukua na kubadilika kwa haraka kwa soko la mawasiliano Tanzania katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Mwaka 2005, kwa kuzingatia mabadiliko ya TEHAMA duniani kote, Tanzania ilianzisha mfumo wa leseni unaozingatia muingiliano wa tekinolojia. Mfumo huo unajulikana kama “converged licencing framework”; kwa kifupi, CLF ambamo, aina nne za leseni zilianzishwa. Hizo ni leseni inayomwezesha mwekezaji kujenga miundombinu na kutoa huduma; leseni inayowezesha kutoa huduma ama kwa kutumia miundombinu anayomilki mtoa huduma au anayokodisha; leseni ya kuwezesha utoaji wa huduma kama vile za mawasiliano ya intaneti, huduma za kifedha kupitia mtandao na leseni kwa ajili ya maudhui ya utangazaji wa televisheni na redio.

Soko la TEHAMA limekuwa kwa idadi ya watumiaji wa huduma hizo, kwa aina mbalimbali za huduma hizo na kwa kuongezeka kwa eneo ambamo huduma mbalimbali zinapatikana; ingawaje idadi ya watumiaji wa simu za mezani imepungua. Kuna laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656 sasa ukilinganisha na laini 2,963,737 mwaka 2005; kama iliyoonyeshwa hapo chini. Idadi ya simu za mezani ni 151, ukilinganisha na 154, 420 mwaka 2005. Watumiaji wa intaneti wameongezake hadi kufikia 11,000,000 Desemba 2014 kutoka 3,563,732 mwaka 2008. Kwa sasa, kuna hamu kubwa ya matumizi ya intaneti na mwelekeo huu utaendelea; hasa kutakapokuwa na ongezeko la mitandao inayowezesha kutoa huduma za intaneti; na kuongezeka kwa mitandao ya jamii.
  1. AINA NA MPANGILIO WA TOZO
Watumiaji wa TEHAMA wanapata aina kuu tatu za huduma, ambazo ni:
  • Huduma za sauti (kuzungumza)
  • Huduma ya ujumbe mfupi wa meseji, kwa kifupi SMS (Short Message System)
  • Intaneti

Wateja walionunua laini au ambao wanatumia huduma za simu kwa kuzungumza imeongezeka kwa asilimia 91 kutoka milioni tatu (3,000,000) mwaka 2005 hadi milioni 32 ( 32,000,000) mwaka 2014. Hii imewezesha huduma za simu kufikia asilimia 97 ya Watanzania ilipofika Desemba 2014; kutoka asimilia 10 mwaka 2005. Kwa upande mwingine, muda wa kuzungumza kwa simu, ukiwa umepimwa kwa dakika zinazotumika, umeongezeka sambamba na ongezeko la idadi ya watumiaji. Umefikia dakika bilioni 41 kutioka dakika milioni 506 mwaka 2005.

Matumizi kwa upande wa meseji, yaani SMS na data pia yameongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka SMS zipatazo milioni 5 mwaka 2005 hadi SMS bilioni 10 mwaka 2014. Watumiaji wa intaneti wanaotumia simu za mkononi sasa wanafikia milioni 10.

Huduma hizi zinatozwa na watoa huduma kwa aina mbili za tozo: Kuna tozo za msingi na tozo mtumiaji anapojiunga na vifurushi. Gharama za kupiga simu zinatozwa kwa shilingi kutokana na dakika mtumiaji atakazotumia kuongea, gharama za kutuma SMS zinatozwa kwa kila ujumbe mfupi unaotumwa na zile za intaneti na data zinatozwa kwa ‘uniti’ ambazo mtu anatumia. Uniti hizi zinaitwa ‘bytes’, kwa mfano, “Megabytes” au kwa kifupi MB na Gigabytes ambazo ni MBs 1,024. Hivyo, matumizi ya intaneti yanatozwa kwa MB au GB mtu anazotumia. Hivi karibuni watoa huduma wametangaza vifurushi vipya ambavyo vimesababisha malamiko kutoka kwa baadhi ya watumiaji.
  1. TOZO ZA MSINGI
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumekuwa na kupungua kwa ujumla kwa tozo za msingi kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali linalofuata, baada ya kuzingatia ongezeko la jumla la bei (inflation). Ni vyema ikazingatiwa kwamba gharama za muingiliano kati ya watoa huduma; yaani kiasi ambacho watoa huduma wanalipana kwa kuwezesha watumiaji wa mitandao mingine kutumia mitandao yao kimekuwa kikipungua. Taarifa hiiinachambua tozo za vifurushi. Iwapo mtumiaji hatajiunga na kifurushi, tozo za msingi zinatumika.

    1. AINA NA MPANGILIO WA VIFURUSHI
Watoa huduma za simu kwa kawaida wanatoa mpangilio wa tozo kwa wateja wao sambamba na tozo za msingi. Vifurushi ni mpangilio ambao mtumiaji anachagua yeye mwenyewe kwa kupenda. Hata hivyo mpangilio huu umetokea kupendwa sana na weatumiaji. Kwa kawaida vifurushi vinauzwa kwa huduma za mazungumzo, za kutuma meseji na za intaneti.
Mtumiaji anaweza kujisajili kutumia kifurushi ama cha siku, wiki au mwezi. Tutachambua mipangilio hii katika majedwali yanayofuata.

  1. VIFURUSHI VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI

3.2.1.1 VIFURUSHI VYA SIKU VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI
Jedwali 1: Idadi ya Dakika, Meseji kwa bei za chini na za juu kwa Siku




Kabla


Baada

Bei (TZS)
Dakika
SMS
MB
Bei
Dakika
SMS
MB
Vodacom
399
4
50
15
499
7
300
8

999
21
1,000
100
999
20
1,000
8
Airtel
399
5
50
15
499
9
300
10

995
40
Bila Kikomo
250
999
24
1,000
10
Tigo
499
7
300
30
649
13
450
8

999
21
1000
100
999
20
1,000
8









Uchambuzi 1:
  • Kuna mabadiliko ya bei na idadi ya dakika na idadi ya meseji. Hata hivyo mabadiko haya sio makubwa.
  • Kuna upungufu mkubwa wa kiasi cha uniti za data, MBs.

3.2.1.2 VIFURUSHI VYA WIKI VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI
Tozo, idadi ya dakika, meseji kwa bei za chini na za juu kwa vifurushi vya Wiki

Jedwali 2: Idadi ya dakika, meseji kwa bei za chini na za juu kwa vifurushi vya Wiki




Kabla

Baada

Bei (TZS)
Dakika
SMS
MB
Bei 
Dakika
SMS
MB
Vodacom
1,999
30
500
100
1,999
29
500
60

4,999
90
1,000
300
9,999
190
1000
60
Airtel
1,995
60
700
175
1,999
34
1,000
70

5,999
200
Bila kikomo
2,000
9,999
200
5,000
70
Tigo
1,999
40
700
300
4,999
91
2,000
60

9,999
250
5,000
1,024
9,999
190
5,000
60

Uchambuzi 2:
  • Kuna mabadiliko ya bei na idadi ya dakika na idadi ya meseji. Hata hivyo mabadiko haya sio makubwa.
  • Kuna upungufu mkubwa wa kiasi cha uniti za data,MBs.

3.2.1.3 VIFURUSHI VYA MWEZI VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI
Tozo, idadi ya dakika, meseji kwa bei za chini na za juu kwa vifurushi vya Mwezi
Jedwali 3: Idadi ya dakika, meseji kwa bei za chini na za juu kwa vifurushi vya Wiki





Kabla

Baada

Bei (TZS)
Dakika
SMS
MB
Bei
Dakika

SMS
MB
Vodacom
10,999
130
500
300
14,999
230

1200
250

29,999
550
2,500
800
49,999
1,000

3,000
250
Airtel
9999
175
5000
400
9,999
175

5,000
300

49,999
1,100
10,000
2048
49,999
1,100

10,000
300
Tigo
9999
200
8,000
1,024
19,999
370

8,000
250

49999
1,200
10,000
4,096
49,999
1,000

10,000
250

Uchambuzi 3:
  • Kuna mabadiliko ya bei na idadi ya dakika na idadi ya meseji. Hata hivyo mabadiko haya sio makubwa.
  • Kuna upungufu mkubwa wa kiasi cha uniti za data,MBs.


    1. VIFURUSHI VYA INTANETI PEKEE.
Kwa ajili ya kulinganisha,vifurushi vya intaneti tu ndivyo vilivyochambuliwa kwa kuwa ndiyo huduma ambayo inatolewa na watoa huduma wenye leseni za kutoa huduma za intaneti.
Jedwali 4. Vifurushi vya Intaneti vya mwezi:



Bei (TZS)
MBs
Bei
Vodacom
2,500
100
25

25,000
Bila kikomo
-
Airtel
12,500
3,000
4

30,000
20,000
2
Tigo
15,000
1,000
15

25,000
Bila kikomo
-
Zantel
6,000
600
10

300,000
Bila kikomo
-

TTCL
28,000
Bila kikomo


Smile
10,500
500
21

1,450,000
200 GB
7

Mpangilio huo wa tozo kwa matumizi ya intaneti kwa mwezi unaonyesha kwamba mtumiaji analipa kidogo anapotumia uniti nyingi zaidi.Kwa hiyo, mpangilio huu unawafaa zaidi wale wenye matumizi makubwa ya intaneti.

  1. HITIMISHO, MAPENDEKEZO NA MAAGIZO:
Kama tulivyoeleza awali kuna aina mbili za toto: Tozo za msingi na tozo za vifurushi. Malalamiko ya hivi karibuni ya watumiaji yameelekezwa kwenye mpangilio na tozo za vifurushi. TCRA imechambua mpangilio wa vifurushi – tozo za zamani na mpya na kugundua kwamba ingawaje baadhi ya watoa huduma wamabadilisha bei, kwa ujumba bei za muda wa kuzungumza na idadi ya meseji hazikubadilika sana. Hata hivyo, kuna upungufu mkubwa kwa idadi ya uniti za data (MBs).

Kwa hivyo, TCRA inaagiza kama ifuatavyo:
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itachukua hatua stahiki za usimamizi kuhakikisha kwamba watoa huduma wanazingatia matakwa ya sheria. Kifungu cha 5 cha Kanuni za tozo (EPOCA Tariff Regulations) za mwaka 2011 kinayataka makampuni ya simu kuwasilisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania gharama mpya wanazokusudia kutoza wateja wao kabla hazijaanza kutumika. Mamlaka itatoa adhabu kila inavyobidi.
  • TCRA inaagiza watoa huduma kuzingatia sheria kila wanapobadilisha bei za bidhaa zao;
  1. Kuziwasilisha kwa Mamlaka kabla hazijaanza kutumika,
  2. Kutoa taarifa za tozo za msingi na vifurushi kwa njia ambayo itaweza kuwafikia watumiaji wa simu za mkonini,
  3. Kupitia upya bei na tozo mpya kwa kuzingatia mapendekezo haya na kuwasilisha kwa Mamlaka kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Kanuni za EPOCA za 2011 kuhusu tozo ( EPOCA (Tariff Regulation of 2011).
  • TCRA inawaagiza watoa huduma kuhakikisha kwamba mabadiliko yoyote yanatekelezwa kidogo kidogo na sio ya ghafla ili kuepuka sintofahamu katika soko;
  1. TCRA inawaagiza watoa huduma kuwapa wateja wao nafasi ya kuchagua mpangilio wa vifurushi tofauti kwa huduma wanazohitaji:
Kifurushi cha mazungumzo, Meseji na Intaneti cha siku, siku saba au mwezi ambacho kinampa mtumiaji uhuru wa kuchagua kiasi ambacho wako tarari kulipia kwa mazungumzo, meseji na intaneti.
  1. Vifurushi vya mazungumzo tu: Hivi navyo kwa siku, siku saba au siku 30 kwa ajili ya watumiaji ambao hawahitaji intaneti na meseji kwa sababu moja au nyingine na wako tayari kulipia vifurushi vya sauti pekee;
  2. Vifurushi cha Meseji (SMS) tu: Kwa watumiaji ambao hawahitaji intaneti au muda wa mazungumzo kwa sababu moja au nyingine, au ambao wanatumia SMS kwa wingi. Hivi nayo viwe kwa siku, siku saba au siku 30 kwa bei ambazo mtumiaji atachagua.
  3. Vifurushi vya Intaneti tu: Kwa watumiaji ambao wanatumia intaneti kwa wingi. Hawa wapewe uhuru wa kuchagua vifurushi vya siku, siku saba au siku 30.
  • TCRA inawashauri watumiaji wa huduma za mawasiliano kuchagua vifurushi na mpangilio wa tozo ambao unafaa kwa matumizi yao. Watumiaji wanatakiwa kudai taarifa kamili kuhusu huduma wanazozilipia na waelewe taarifa za watoa huduma kuhusu bei na tozo, ikiwa ni pamoja na vigezo na masharti ya huduma. Mtumiaji asiporidhishwa na huduma anayopata anatakiwa alalamike – kwanza kwa mtoa huduma wake, na asiporidhika na ufumbuzi awasilishe malalamiko yake TCRA.
  • Watumiaji wanashauriwa kuchukua fursa ya soko huria la mawasiliano nchini kama nafasi ya kulinganisha huduma na bei za watoa huduma na vifurushi wanavyouza kabla ya kuamua kujiunga na kifurushi chochote au huduma yoyote.
  • Watumiaji wa simu janja zinazowezesha matumizi ya huduma nyingi, maarufu kama “smart phone”, kuwa makini wakati wa kuzitumia. Wahakikishe kwamba wanazima maeneo ambayo yanaweza kutumia data hata kama wakati huo hawatumii vifurushi vya data walivyonunua kwenye vifurushi.
Kwa taarifa zaidi, wasiliana na TCRA, Na. 20 Barabara ya Sam Nujoma, Dar Es Salaam. SL.P 474 Dar Es Salaam 14414. Barua pepe: dg@tcra.go.tz

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

23 Februari 2015


EmoticonEmoticon