Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo asubuhi amelazimika
kusitisha shughuli za bunge baada ya wabunge kutaka serikali
kuahirisha mchakato wa kura ya maoni pamoja na kutoa taarifa ya
uandikishwaji wa wapigakura kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa
BVR.
Wakichangia
hoja bungeni Mbunge wa Kisarawe Mh. Suleiman Jaffo na Mbunge wa
Ubungo Mh. John mnyika wametaka suala hilo lijadiliwe kama dharura na
kutolewa majibu na serikali kuhusu hatama ya mchakato huo.
Taharuki
ilizuka baada ya Spika wa Bunge hilo Mhe. Makinda kutaka kuzitupilia
mbali hoja hizo. Wabunge walianza kupiga kelele kutaka majibu ya
serikali papo hapo na ndipo Spika wa bunge alilazimika kuhairisha
kikao hicho mpaka jioni ambapo leo ni kikao cha mwisho cha bunge
hilo.
“ Mnyika
“ Nimesimama kupata Idhini kwa mujibu wa kanuni kuomba shuguli za
mbunge zisitishwe na badala yake tujadili zoezi la uandikishwaji
kwani mpaka sasa zoezi halijakamalika hata kwa mkoa mmoja, hivyo
Waziri mkuu kwakuwa yupo hapa Bungeni atupe majibu nini kinaendelea”
Amesema Mnyika
Spika
“Hoja hii na ile ya kwanza zinafanana, majibu mtajibiwa baadae
katika kikao cha jioni” Alisema spika. Aidha wabunge wa Upinzani
walionesha nia ya kutaka kujua hivyo kupiga kelele kwakusema “Tuna
taka Majibu” hali iliyopelekea spika wa bunge kuahirisha Bunge hadi
jioni.
Bunge
la jioni tunatarajia Mhe. Mizengo Pinda Waziri mkuu wa Tanzania kutoa
tamko la serikali nini hatma ya mchakato wa kupigia kura katiba
inayopendekezwa.
Kura
ya maoni inategemewa kupigwa tarehe 30 mwei wa 4, 2015 mwaka huu
licha ya kutokuwepo kwa uboreshaji wa daftari la kupiga kura kwa
kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa BVR.
EmoticonEmoticon