MHE. DEO FILIKUNJOMBE AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NDEGE



Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la ludewa kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi ccm mhe. deo filikunjombe na wengine watatu wamefariki dunia katika ajali ya chopa iliyotokea eneo la hifadhi ya selous

Akidhibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamishna wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi poul chagonja amesema ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria wanne wakitokea dar es salaam kuelekea njombe na waliotambuliwa mpaka sasa ni rubani wa ndege hiyo capten willium silaa na deo filikunjombe

Kamishna chagonja amesema jeshio la polisi limaendelea na uchunguzi wa ajali ya ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y DKK unaendelea na kuwa abiria wengine wawili bado hawajatambuliwa kwa majina yao.
sauti ya kamishna chagonja akielezea zaidi





Mhe. deo filikunjombe amezaliwa tarehe 4 mwezi wa 3 mwaka 1972,amekuwa mbunge wa ludewa kwa mwaka 2010 mpaka 2015. akiwa bungeni mhe. filikunjombe amewahi kuchangia mara 43.


Katika kipindi chake cha ubunge amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwapamoja nakuwa makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma na baadaye kamati ya hesabu za serikali chini ya mwenyekiti wake zitto kabwe, na miongoni mwa mambo ambayo atakumbukwa zaidi ni namna alivyoshughulikia sakata la tegeta escrow.

Kwa kushirikiana na wajumbe wa kamati yake pamoja na ripoti ya cag, kamati hiyo ilitoa taarifa bungeni mwezi novemba mwaka jana, ambayo ilipelekea kung'oka kwa mawaziri wawili na mwanasheria mkuu wa serikali.

Mtu mwingine aliye poteza maisha katika ajali hiyo ni Kepteni wa ndege hiyo bwana Willium Slaa. 


EmoticonEmoticon