Mwenyekiti
wa tume ya uchaguzi zanzibar salim jecha salim ametangaza kufutilia
mbali matokeo ya uchaguzi visiwani humo kwa madai kuwa kumekuwepo kwa
kura nyingi kuliko idadi iliyopo kwenye daftari la wapiga kura.
Akitangaza
suala hilo mwenyekiti wa zec amesema kumetokea kuwepo kwa dosari
nyingi kwenye upigaji kura jambo ambalo amelitaja kuwa sio wa haki.
"Kumegundulika
kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa
baadhi ya vituo vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura
wa kituo husika." amesema salim jecha
Amesema
hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba "baadhi ya
wapiga kura hawakwenda kuchukuwa vitambulisho vyao vya kupigia kura".
Wakati
huo huo, mgombea wa urais kupitia
tiketi ya chama cha chadema na ukawa edward lowassa amesema
hakubaliani na matokeo ya uchaguzi wa urais yanayoendelea kutolewa na
tume ya uchaguzi nchini tanzania nec.
Lowasa ametoa madai kuwa kuna udanganyifu uliofanyika
nakuwa kura za chama hicho zimepunguzwa katika vituo vingi vya
kupigia kura, pia lowassa ameongezea kuwa maeneo yote ambayo walipata
ushindi matokeo yamechelewa kutajwa.
EmoticonEmoticon