Ikiwa imebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu katika hali isiyo ya kawaida watu wanne wasiofahamika itikadi zao za kisiasa wamekamatwa na wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) kwa madai ya kupita katika kata za manispaa ya morogoro na kudai shahada za wapiga kura kwa nguvu na kuanza kuorodhesha majina ya wananchi na namba zao za simu
kwa upande wananchi mashuhududa waliokumbana na watu hao katika harakati za kuwaandikisha wapiga kura majina wameeleza jinsi watu hao walivyokuwa wakifanya zoezi hilo kwa kudai kwa lazima shahada za kupigia kura ambapo baadhi ya watu walikubali na wengine wafikisha jambo hilo kwa afisa mtendaji wakata na wananchi waliamua kuungana na kuwakamata na kisha kuwapeleka katika kituo cha polisi cha mji wa morogoro.
Akitolea ufafanuzi kuhusiana na suala hilo msimamizi wa uchaguzi jimbo la morogoro mjini bi theresia mahongo amesema kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai na kwamba adhabu yake ni faini kati ya shilingi laki moja hadi laki mbili au kifungo cha miaka miwili ama vyote na kuwaonya wananchi kuacha kufanya hivyo nikosa la jinai
EmoticonEmoticon