Mwenyekiti
Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amesema kuwa
atashirikiana na jeshi la Polisi nchini Tanzania Kutoa zawadi ya
shillingi millioni kumi kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa watu
waliyomkata mkono Munghu Mugasa mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi
katika kijiji cha Buhekela Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora pamoja na
kumuua mume wa mama huyo nakujeruhi watoto wao wawili.
Dkt. Mengi ameyaeleza hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya habari na kueleza kuwa IPP itachukua jukumu la kuwasomesha watoto wawili wa familia hiyo ambao baba yao ameuwawa na mama yao kuachwa na ulemavu huku akilitaka jeshi la Polisi nchini kuhakikisha kuwa wanawatia nguvuni wale wote waliohusika na tukio hilo.
“Unge jiskiaje endapo aliye uwawa angekuwa ndugu yako ama aliye katwa mkono ni ndugu yako? Inasikitisha sana. Mimi sina la kufanya ila naomba sana serikali na hasa jeshi la polisi Mkoa wa Tabora kufanya msako kuwakamata waliohusika na tukio hili lakusikitisha” Amesema Dkt Mengi.