BUNJU SISTERS GROUP INAKARIBISHA WANACHAMA WAPYA


Kikundi cha Bunju Sisters Group kimekuwa kikikutana kila mwisho wa mwezi kwaajili ya kupea taarifa mbalimbali za chama, mapato na matumizi pamoja na mipango ya baadae ya kikundi chetu

Kuanzia kushoto ni Wendy muweka hazina , wapili ni Suzan Nzota Katibu na wamwisho ni Loyce Joseph mwenyekiti wa kikundi
Japo tumekuwa na misukosuko mbalimbali ikiwemo ya misiba ya wanafamili wa wanachama wetu, wengine kutengana na kikundi kuelekea vyuoni kwa masomo pamoja na ubize wa kazi za kila siku lakini Umoja na urafiki bado unadumu kati yetu

Kutoka kushoto ni Bibiana, Suzy na Janeth Jackson

Pole kwa Janeth Jackson aliye mpoteza Mume wake Kipenzi, Pole kwa Rosemery aliye fiwa na baba yake kipenzi kwa upande mwingine Hongera kwa Bibiana aliye mwozesha mdogo wake na Lucy aliye baatika kupata mtoto wa kiume mungu awape maisha marefu sana wana kikundi



Mara nyingi tumekuwa kwenye vikao vya usiku, kutoka out kubadilishana mawazo na mara zingine tunatembeleana ili kuzidisha mshikamano wetu. Tume weza kukopeshana na kusaidia kwenye matatizo mbalimbali kama msiba na harusi na kiuchumi.

Kutoka kushito ni Janeth, Loyce Joseph, Bibiana na Lucy
Mwenyekiti wa Bunju Sisters Group anapenda kuwkaribisha kina dada wote wenye nia ya maendeleo na kusaidana, kupata marafiki katika eneo la Bunju kuwasilina nasi kupitia Simu no. 0659 269416 kwani huu ni muda wa kukaribisha wanachama wapya. Vigezo na masharti nivya kawaida Karibu.


EmoticonEmoticon