Wakala
wa nishati vijijini REA, imeanza kufanya uchunguzi kuhusiana na
tuhuma kuwa baadhi ya wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini
wamekuwa wakichukua rushwa kutoka kwa wateja ili kuwaunganishia
huduma hiyo.
Mkurugenzi
mkuu wa REA Dkt. Lutengano Mwakahesya, amesema hayo katika mahojiano
na East Africa TV, ambapo amewataka wananchi kutokubali kutoa rushwa
kwa kampuni zinazounganisha huduma hiyo vijijini.
“Kwa
nini uchukue rushwa kwa mwananchi wa kijijini ambaye maisha yake ni
bado yana mahitaji mengi, hili suala sio zuri kabisa na Waziri wetu
(Mhe. Sospeter Muhongo) ameshatoa kauli kuwa nikinyume cha taratibu”
amesema Lutengano
Aidha
Dkt Lutengano ameongeza kuwa watumishi wa kampuni zilizobainika
kujihusisha na rushwa, watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na
tuhuma zao kufikishwa kwenye taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
TAKUKURU, jeshi la polisi na kwa mamlaka ya udhibiti wa manunuzi
katika sekta ya umma—PPRA, huku
Hatahivyo
Dkt. Lutengano amesema nihaki kisheria kwa mwananchi kulipwa fidia
kabla ya miradi ya umeme kupita kwenye maeneo yaohivyo kuzidi
kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali kupitisha umeme
kwenye maeneo yao huku dhathmini ikifanyika ya kuwapa fidia wale
ambao mazao yao yameharibiwa kwa kupisha miradi ya umeme.
EmoticonEmoticon