Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa
kampeni za kugombea kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia
Chama cha Mapinduzi (CCM) hazijaanza rasmi.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa vitendo vya baadhi ya watu kuanza kampeni
kabla ya wakati wake ni moja ya mambo yanayosikitisha.
Hata
hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa suala hilo zima limekabidhiwa kwa
Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara) Mzee Philip Mangula
ambaye atalisimamia jambo hilo na kulishughulikia.
Rais
na Mwenyekiti wa CCM alikuwa anazunguza na wajumbe wa Halmashauri ya
CCM ya Mkoa wa Mbeya kwenye Ukumbi wa CCM mjini Mbeya.katika ziara ya
kikazi ya siku mbili mkoani Mbeya.
Maandalizi
Bunge La Katiba, Rais akagua Ukumbi wa Bunge Dodoma
Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumamosi, Februari Mosi, 2014, amekagua na
kuridhishwa na kazi na kasi ya marekebisho yanayofanywa katika Ukumbi
wa Bunge mjini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya Vikao vya Bunge Maalum
la Katiba linaloanza baadaye mwezi huu.
Rais
Kikwete amesimama kwa muda mjini Dodoma kujiridhisha na mwenendo wa
maandalizi ya Bunge Maalum akiwa njiani kwenda Mbeya ambako atafanya
ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais
Kikwete amekagua Ukumbi huo na huduma nyingine muhimu kwa ajili ya
vikao hivyo ikiwa ni pamoja na bwalo la chakula kwa kiasi cha dakika
45 na kuvutiwa na mwenendo wa kazi na kasi ya marekebisho kwenye
ukumbi huo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa William Lukuvi
amemhakikishia Rais Kikwete kuwa kazi yote ya kufunga viti na vipaza
sauti, ambavyo vitatumia mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya kadi,
ndani ya ukumbi huo itakuwa imekamilika ifikapo Februari 10, mwaka
huu, siku tisa kuanzia sasa.
Bunge
Maalum litakuwa na wajumbe 645 ambao ni Wabunge wa sasa wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar na Wajumbe 201 ambao watateuliwa na Rais kutokana na
mapendekezo ya makundi mbali ambayo yanatajwa katika Sheria ya
Marekebisho ya Katiba.
EmoticonEmoticon