Chama
cha wansheria wanawake nchini Tanzania TAWLA, kimeanzisha utaratibu
wa msaada wa namna jamii inavyoweza kupata huduma za kisheria kwa
kuanzisha utaratibu wa wanasheria wasaidizi.
Mwenyekiti
wa TAWLA Bi. Aisha Bade amesema wanasheria wasaidizi watakuwa
wanaelekeza jamii namna ya kupata huduma za kisheria hasa kwa makundi
yenye uhitaji wakiwemo wanawake, watoto, wajane, waathirika wa
ubakaji pamoja na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa
mujibu wa Bi. Bade, mpaka sasa TAWLA imeshafundisha na kuandaa
wanasheria wasaidizi 412 waliosambazwa maeneo mbali mbali nchini,
ambao uwepo wao utapunguza garama ya kupta huduma za kisheria pamoja
na pengo la uhaba wa huduma hiyo katika jamii.
“Mara
nyingi watu wananyimwa haki au wanakosa hki kwa kukosa misaada wa
kisheria kutokana na upatikanaji wake ni gali na iko mbali na jamii
hivyo hawa wasaidizi wa kisheria watatusaidia kuwafikia jamii kwa
haraka zaidi n a bila garama yoyote” amesema
Pamoja
na kuazishwa kwa huduma hiyo bado vongozi wa serikali hasa kwenye
ngazi za mikoa hawatoa ushirikiano wakutosha kwa wasaidizi wa
kisheria hali inayo rudisha nyuma jitihada za masuala ya kisheria,
hivyo wananchi na viongozi wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatoa
ushirikiano ili tuwe na taifa lenye haki na usawa.
EmoticonEmoticon