Wizara ya afya na ustawi wa jamii
nchini Tanzania imebaini asilimia 13.7 ya wananchi wanadalili ya
ugonjwa wa kisukari kwa Tanzania bara hali inayosababishwa na uvutaji
wa sigara au tumbaku na unywa wa pombe kupita kiasi pamoja na kutokufanya mazoezi na
lishe duni.
Utafiti huo pia umeonyesha kuwa
asilimia 14.5 wanakunywa pombe kila sikuhuku asilimia 36 wanavuta
sigara. Kuhusu masuala ya uzito kupita kiasi ni asilimia 24 wanauzito
usio hitajika huku asilimia 30 wameonekana kuwa na ongezeko la
msukumo wa damu.
Akizungumza wakati akizindua
utoaji wa huduma za bure zinazotolewa na Jeshi la wananchi wa
Tanzania(JWTZ) kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya jeshi hilo
katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam kwa muda wa siku
3, Kaimu mkurugenzi wa tiba wa wizara hiyo Dr.Ayoub Magimbu
amewataka wananchi kuipunguza matumizi ya vitu ambavyo vitahatarisha
maisha yao.
Naye Brigedia General Dennis
Jenga ambaye ni mkuu wa tiba JWTZ amesema jeshi hilo linajivunia
kwakuwa na madaktari zaidi ya 200 suala ambali linaiwezesha jeshi
hilo kuhudumia watendaji wake na wananchi kwa ujula.
Brigedia General Jenga ameongeza
kuwa kuanzia hii leo katika viwanja vya mnazi mmoja watatoa huduma za
afya bure ikiwa ni maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya
jeshi hilo. Nakuwataka wananchi kuhudhuria viwanjani hapo kwaajili ya
kupata huduma bure.
Huduma zitakazo tolewa viwanjani
hapo nibamoja na upimaji wa VVU;Uchangiaji damu wa hiari magonjwa ya
kinywa na meno magonjwa ya mamcho pamoja na kufanya vipimo vya uzito
na kujua kiwango cha damu mwilini.
EmoticonEmoticon