RAIS alie maliza mudawake nchini Kenya Bwana Mwai Kibaki ambaye pia alitunukiwa barabara lenye jina lake hivi karibuni jijini Dar es salaam, Aewatakia heri Rais mteule Bwana Uhuru Kenyatta na makamu wake Bwana Willium Ruto
kwa ushindi wao, hii leo katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Nairobi
Kutoka Kushoto ni Rais mpya wa Kenya bwana Uhuru Kenyatta, katika ni Rais Mstaafu Mwai Kibaki Kulia ni Willium Ruto |
Bwana Mwai Kibaki amewapongeza wawili hao, kwa ushindi kama
ilivyotangazwa na tume huru ya uchaguzi wan chi hiyo (IEBC), Huku akiwatakia
heri katika uongozi wao
Licha ya Raila Odinga ambaye alikuwa mgombea wa urais Kukimbilia
mahakamani kupibnga matokeo hayo, Bwana Uhuru Kenyatta amezidi kupata mibaraka
kutoka kwa viongozi wa Dini mbalimbali ilikuweza kuongoza nchi vyema
Uhuru Kenyatta akiombewa katika kanisa katoliki la Gatundu hii leo |
Hata hivyo bado malalamiko mengine yanaendelea kutolewa na
watu mbalimbali juu ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, ambapo
mdogo wake Rais Barack Obama, bwana Malik Obama naye ameitupia lawama tume ya
uchaguzi ya nchihiyo IEBC kutokana na kura za eneo la SIAYA huko nchini Kenya